The House of Favourite Newspapers

FT: FINALI YA NDONDO CUP, KIVULE 0-1 MANZESE KUTOKA UWANJA WA BANDARI, DAR

Mchezo wa fainali ya Ndondo Cup kwenye uwanja wa Bandari, Tandika uliopo katika wilaya ya Temeke.

 

Ni timu mbili zenye profile zinazofanana, timu zote ni mpya kabisa kwenye mashindano, zote zimeingia msimu huu na kuanzia hatua ya awali kabisa ya mashindano (hatua ya awali inashirikisha timu 64).

HATUA YA AWALI

Manze United
Walishinda michezo miwili wakatoka sare mchezo mmoja, wakafanikiwa kuongoza kundi lao wakiwa na alama 7
Kivule United

Walishinda mechi mbili wakafungwa mechi moja wakafuzu wakiwa vinara wa kundi lao kwa pointi 6.

HATUA YA MAKUNDI

Manzese Unite
Ilikuwa Kundi B pamoja na Ilala UTD, Makumba na Kibada One.  Walishinda mechi mbili katika hatua hii na kutoka sare mchezo mmoja ikaongoza kundi ikiwa na pointi 7  na kufanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora.

Kivule United

Iliangukia Kundi F kundi moja na Mpakani Kombaini, Mtoni City na Buguruni United. Ilishinda michezo miwili katika kundi hili na kupoteza mechi moja. Ikamaliza katika nafasi ya pili katika kundi lake ikiwa na pointi 6 nyuma ya Mpakani Kombaini iliyomaliza ikiwa na pointi 7.

HATUA YA 16 BORA

Manzese United waliwatoa majirani zao Mabibo Market kwa kuwafunga goli 1-0 na kufuzu hatua ya robo fainali.

Kivule United walifanikiwa kufuzu robo fainali kwa kuwatupa nje ya mashindano wakongwe Kauzu FC kwa penati 3-1 baada ya mechi yao kumalizika 0-0 ndani ya dakika 90.

ROBO FAINALI

Manzese walipita baada ya ushindi wao wa penati 4-2 dhidi ya UV Temeke baada ya sare ya kufungana 2-2 ndani ya dakika 90.

Kwa upande wa Kivule United, katika hatua hii walicheza na Makuburi FC mchezo ambao ulimalizika 0-0 ambapo Kivule walishinda kwa penati 4-2.

NUSU FAINALI

Manzese iliitoa Banda FC kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya suluhu na kukata tiketi ya kucheza fainali ya Ndondo Cup.

Kivule wamefanikiwa kuingia fainali baada ya ushindi wa matuta 2-0 dhidi ya Faru Jeuri kufuatia sare ya bila kufungana (suluhu).

FAINALI

Comments are closed.