The House of Favourite Newspapers

Kauli ya Kwanza ya Mrithi wa Sirro, Kanda Maalum Dar -(VIDEO)

0
Kamanda mpya wa Kanda maalum ya Dar es Salaam, Mambosasa akizungumza na waandishi wa habari.
Wanahabari wakiendelea kumsikiliza kwa makini Kamanda huyo mpya wa polisi.

Mrithi wa Simon Sirro, Lazaro Benedict Mambosasa, ambaye ni kamishina mwandamizi msaidizi wa jeshi la polisi, leo amezungumza kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe.

Mambo sasa amesema, amejitokeza mbele ya waandishi wa habari ili wamfahamu na aweze kuwapatia mawasiliano yake ikiwemo namba ya simu. Pia, amewaombaa waandishi wa habari wampe ushirikiano katika utoaji wa habari. Amedai anachoomba kutoka kwa waandishi wa habari ni taarifa tu. hususani taarifa juu ya masuala ya uhalifu.

Katika hotuba yake hiyo, alielezea nafasi mbalimbali ambazo amehudumu mpaka hapo alipo hivi sasa.

“Ninawaombeni sana ushirikiano… najua nguvu ya kalamu mliyonayo, tukishirikiana nina imani Dar es salaam tutaiweka sawa.” alisema.

Alitaja namba zake mbili ambazo ni 0756616777 na 0753 616 277 huku akieleza kuwa anapatikana usiku na mchana. Mkutano ulimalizika kwa waandishi wa habari kupewa nafasi ya kuuliza maswali.

Kamanda Mambosasa amejieleza kwamba anao uzoefu mkubwa wa kazi hiyo kwani amewahi kuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Tarime-Rorya, alikofanya kazi kwa muda wa miaka miwili.

(PICHA: DENIS MTIMA/GPL)

JOB OPPORTUNITIES AT MUHIMBILI, AUGUST 2017

 

VIDEO: Kauli ya Kwanza ya Mrithi wa Sirro, Kanda Maalum Dar

Leave A Reply