The House of Favourite Newspapers

Gerson Msigwa; Chanjo ya UVIKO-19 Kupelekwa Vijijini – Video

0

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Septemba 12, 2021 akizungumza na Watanzania katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu Utekelezaji wa Serikali katika Sekta Mbalimbali, Mkutano huo unafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

 

Msigwa amesmea Serikali inaendelea kutoa elimu na kuwahamasisha Watanzania kuchukua tahadhari pamoja na kupokea chanjo, Chanjo imeendelea kutolewa ambapo zaidi ya Watanzania 345,000 wameshapata chanjo.

 

“Kampeni kubwa inayofanyika sasa ni kupeleka chanjo vijijini ili Watanzania wengi waweze kuipata. Mwishoni mwa Septemba au mwanzoni mwa Oktoba 2021 tutakuwa na “Wiki ya Uchanjaji” ambapo viongozi wetu wa nchi nzima watapata chanjo” amesema Gerson Msigwa

 

Pia amesema Kuna baadhi ya maeneo yanapata changamoto ya kukatika kwa umeme, ni kwa sababu ya kazi kubwa inayoendelea ya kubadilisha nguzo zilizooza, na hivi sasa Serikali imeamua kuweka nguzo za zege kwa lengo la kutatua changamoto hiyo.

 

“Hali ya uzalishaji wa umeme kwenye nchi yetu ni nzuri, tunaendelea kuzalisha zaidi ya Megawati 1,600, mahitaji yetu ni Megawati 1,200 na tuna ziada ya Megawati 400”

 

“Kuna sehemu chache nchini yetu ambazo bado hazijafikiwa na Gridi ya Taifa, ikiwemo mkoa wa Kigoma, wiki iliyopita wananchi wa Kigoma walipata changamoto ya mgao wa umeme, Waziri wa Nishati, Medard Kalemani alikwenda kufanyia kazi changamoto hiyo”

 

“Kuna baadhi ya maeneo yamepata changamoto ya kukatika kwa umeme, ni kwa sababu ya kazi kubwa inayoendelea ya kubadilisha nguzo zilizooza, na hivi sasa Serikali imeamua kuweka nguzo za zege kwa lengo la kutatua changamoto hiyo”

 

”Serikali moja ya vitu ambavyo inaviangalia ni kuhakikisha tunakuwa na wiki ya uchanjaji. Utaratibu huu sasa unaandaliwa bila shaka mwishoni mwa mwezi wa 9 au mwanzoni mwa mwezi wa 10, tutakuwa na wiki ya uchanjaji”

“Tunataka mtandao uwafikie Watanzania kama ambavyo umeme umewafikia Watanzania wengi mpaka wanaoishi kwenye nyumba za tembe

 

“Tunataka Mtanzania akipata hiyo njia ya mawasiliano katika nyumba yake aweze kupiga simu, kupata intaneti na kutumia televisheni kupitia mtanda”

 

“Hivi karibuni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imekubaliana na TANESCO kwamba itatumia shirika hilo la umeme kusambaza Mkongo wa Taifa”

 

 

Leave A Reply