LIVE: Mwili wa Rais Mugabe Ukiagwa Zimbabwe

MWILI wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe na muasisi wa taifa hilo, Robert Gabriel Mugabe, umeagwa leo Alhamisi, Septemba 12, 2019 katika Uwanja wa Taifa wa Rufaro jijini Harare nchini humo ambapo maelfu ya wananchi wakiongozwa na Rais wa nchi hiyo, Emerson Mnangagwa wamejitokeza kutoa heshima zao za mwisho.

Mugabe alifariki wiki iliyopita nchini Singapore alikokuwa akipatiwa matibabu na mwili wake kuwasili Zimbabwe jana kwa ajili ya kuagwa na mazishi ambayo yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo ( kwa mujibu wa familia lakini siku haijatajwa) kijijini kwao, Kutama.


Loading...

Toa comment