The House of Favourite Newspapers

Watatu Wakamatwa na Meno ya Tembo, Polisi Yakusanya Bilioni 1.2 – Video

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 1.2 katika kipindi cha kuanzia mwaka mmoja kuanzia Novemba 1, 2017 hadi Novemba 23, 2018 kutokana na makossa 36,778 ya barabarani.

 

Hayo yamesemwa leo Ijumaa na Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, SACP Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam wakati akitoa ripoti ya utendaji wa Jeshi hilo ambapo ameeleza kwamba waliokamatwa kwa makosa ya barabarani na kutakiwa kulipa faini ndani ya siku 7 wanatakiwa kutii utaratibu huo.

 

“Kuzidisha muda wa kulipa deni hilo ni ukiukaji wa taratibu na magari yatakapokamatwa Jeshi lataka lisilaumiwe…… Ambaye atafanya Maandamano, Marathon na Matembezi ya Hisani bila kupata kibali, tutazuia bila kujali ni taasisi gani inayofanya hayo,” amesema Mambosasa.

 

Mambosasa amesema Jeshi hilo linawashikiliwa watu 3 kwa tuhuma za kukutwa na vipande 18 vya meno ya Tembo. Watuhumiwa hao ambao walikamatwa katika maeneo ya Yombo Makangarawe, hivi karibuni, wanadaiwa walikuwa wamevificha vipande hivyo kwenye mabegi mawili ya mgongoni na kwamba bado wanaendelea kuhojiwa.

 

Pia, amesema watu wawili wanaodhaniwa kuwa majambazi wanaofanya uhalifu kwa kutumia pikipiki na gari wamekamatwa. Wanatuhumiwa kwa utekaji wa waendesha Pikipiki na kupora Pikipiki

 

Aidha, Mambosasa ametoa tahadhari kuhusiana na taasisi bandia zilizojitokeza kupitia Mitandao kwa mwamvuli wa kutoa mikopo ambao wanatumia majina ya viongozi na wafanyabiashara. Amesema wamekuwa wakitumia majina ya Jokate Mwegelo, Reginald Mengi na Mohammed Dewji.

VIDEO: MSIKIE MAMBOSASA AKIFUNGUKA

Comments are closed.