The House of Favourite Newspapers

SAMIA SULUHU AZINDUA MRADI WA KUIMARISHA USIMAMIZI MALIASILI

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Jumatatu, Februari 12, 2018 amezindua rasmi Mradi wa Kuimarisha Usimamizi wa Maliasili, Ukanda wa Kusini mwa Tanzania.

Katika hafla hiyo ya kihistoria iliyofanyika katika Viwanja vya Kihesa, Kilolo mkoani Iringa, viongozi mbalimbali wamehudhuria wakiwemo Waziri mwenye dhamana ya maliasili na utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi maatibu wakuu, wakuu wa mikoa na wilaya na wengine.

Mradi huo ambao umegharimu pesa kiasi cha Tsh. Bilioni 340, umedhaminiwa na Benki ya Dunia kwa mkopo wenye masharti nafuu.

 

“Sekta ya utalii ina mchango mkubwa wa kukuza uchumi wa nchi yetu, inaingiza pesa nyingi za kigeni, inatengeneza ajira nyingi kwa vijana wetu. Kama mnavyofahamu, ukanda huu wa Kusini una vivutio vingi vya utalii lakini kutokana na changamoto za miundombinu zikiwemo barabara, vingi vyao havuifikiki kirahini.

“Serikali itahakikisha inajenga miundombinu imara ili kuvutia watalii kuja Kusini kutembelea maliasili zetu. Hivyo wizara zinafanya jitihada ya kuhakikisha mikakati ya serikali kukuza vivutio hivi vya utalii inatekelezwa,” alisema Samia.

 

Global TV Online Ilikuwa LIVE, fuatilia tukio hilo hapa

Comments are closed.