Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia kwa pamoja (Picha na Maktaba)
Full Time: Yanga 2 – 0 Mwadui, Mfungaji wa Yanga ni Obrey Chirwa mabao yote mawili.
Dakika ya 89: Dida anatoka na kuidaka vizuri krosi ya Nonga ambaye aliuwahi mpira pembeni
Dakika ya 87: Yanga wanaendelea kulisakama zaidi lango la Mwadui
Dakika ya 85: Gooooooooooooooooooooooooo! Yanga wanapata bao la pili mfungaji ni Obrey Chirwa
Dakika ya Mabadiliko : Amisi Tambwe anatoka anaingia
Dakika ya 74: Mwadui wanashambulia wanakosa bao
Goooooooooooooooooooooooo! Chirwa anaiandika Yanga bao safi hapa baada ya shuti la Msuva, Kado akatema na yeye akaunganisha
Dakika ya 67: Yanga wanapata nafasi ya kufunga, wanakosa wanapiga kizembe
Dakika ya 64: Mabadiliko Yanga wanamtoa Haruna na nafasi yake inachukuliwa na Chirwa
Dakika ya 63; Bado Yanga 0-0 Mwadui
Dakika ya 61: Mwadui wanakosa goli na Dida anadaka kwa kulala
Dakika ya 58: Yanga wanacheza vizuri na kufanya mashambulizi kadhaa lakini wanakosa umakini langoni mwa Mwadui FC
Dakika ya 57: Yanga wanashambulia kwa kasi
Dakika ya 52: Kaseke anakwenda benchi nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin
Kadi Dakika ya 49 Mwamuzi Jonesia Lukyaa anamlamba Cannavaro kadi ya njano kwa kucheza rafu
Dakika ya 46, Yanga wanaanza kwa kasi, wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Mwadui. Goal kick
Kipindi cha pili Kimeanza ndani ya Uwanja wa Taifa
Mapumziko
Dakika za nyongeza, Msuva anapiga shuti kali linaloishia kwa mlinda mlango Shabani Kado.
Dakika ya 44: Zimeongezwa dakika 2 kuelekea mapumziko
Dakika ya 42: Kipa wa Yanga, Dida anacheza faulo mchezaji wa Mwadui
Dakika 41: Yanga wanapata kona kuelekea katika lango la Mwadui, Yanga wanakosa gori
Dakika ya 37: Bado hakuna aliyefumania nyavu mpaka sasa.
Dakika ya 31, Mustappha anatoa mpira nje, inakuwa kona langoni kwa Mwadui FC
Dakika ya 26 sasa, Mwadui FC wanaonekana wamejipanga kujilinda sana na mashambulizi ya kushitukiza
Dakika ya 21: Mwadui wanapata faulo
Dakika ya 20: Yanga SC 0-0 Mwadui FC
Dk 18, Mwadui FC wanaonekana wakiwa wametulia, angalau wanagonga hata pasi tano. Lakini Yanga wanaendelea kufika langoni mwa Mwadui FC
Dk 12, Kado yuko chini akipatiwa matibabu
Dakika ya 12 Shaaban Kado anafanya kazi nzuri ya kuokoa michomo kadhaa ya washambuliaji wa Yanga.
Dakika ya 9, Kado anafanya kazi ya ziada kuudaka mkwaju wa Msuva. Yanga wanaendelea kushambulia kwa kasi kutafuta bao la kuongoza
Hali ya Hewa ni murua kabisa kutoka Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam. Dakika ya 6 bado Yanga 0-0 Mwadui
Kikosi cha timu ya Mwadui Fc
Dk 5, Msuva anauwahi mpira wa krosi ya Juma Adul lakini anashindwa kulenga lango
Dk 4, krosi maridadi ya Mwinyi Haji lakini Kado anaruka juu na kupangua
Dakika ya 1 Mechi imeanza Mwadui wakianza kusukuma mashambulizi ingawa, lakini Yanga wanakuwa wa kwanza kufika kwa Mwadui na kipa Shabani Kado anaondosha hatari
Kikosi cha Mwadui: Mobby, Kado, Cholo, Mustapha, Ndeule, Kabunda, Khalphani, Awadhi, Nonga Salim Khamis na Seseme.
Kikosi cha Yanga SC
Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam
Comments are closed.