The House of Favourite Newspapers

LIVE UPDATES: Hali Ilivyo Kenya, ‘Raila Odinga Akijiapisha Kuwa Rais’

NAIROBI: Hali ya wasiwasi imetanda nchini Kenya baada ya kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo Bwana Raila Odinga, kushikilia kuwa ataapishwa leo kama rais wa nchi hiyo.

Muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) umesema hafla hiyo itafanyika katika uwanja wa Uhuru Park, Nairobi. Baada ya sherehe hizo kuahirishwa mwezi uliopita, muungano mkuu wa upinzani nchini humo-NASA, bado unaendelea na msimamo wake wa kuwaapisha viongozi wake Raila Odinga na Stephen Kalonzo Musyoka, kama Rais na Makamu wa rais wa Jamhuri ya Kenya.

Maofisa wa Polisi walifika asubuhi na mapema katika Uwanja wa Uhuru Park, Nairobi unaopanga kutumiwa na muungano wa Nasa kwa shughuli ya kumuapisha Bw Odinga.

Kituo cha habari cha kibinafsi cha Citizen kimeripoti kuwa maafisa wa polisi wameamrishwa kuondoka katika uwanja wa Uhuru Park.

Mabasi ya wafuasi wa upinzani yazuiwa Voi

Mabasi matatu yaliyokuwa yanawasafirisha wafuasi wa upinzani waliokuwa wanaelekea Nairobi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa kiongozi wao Raila Odinga yamekamatwa na maafisa wa polisi katika mji wa Voi, katika barabara ya kutoka Mombasa kwenda Nairobi.

Mji wa Voi unapatikana takriban kilomita 330 mashariki mwa mji huo mkuu wa Kenya.

Afisa wa polisi amewaambia wanahabari kwamba madereva wa mabasi hayo walikuwa wamevunja sheria kadha za barabarani.

Wafuasi wa upinzani waanza kuingia Uhuru Park

Wafuasi wa upinzani nchini Kenya wameanza kuingia uwanja wa Uhuru Park baada ya polisi kuondoka.

Baadhi wanazunguka uwanja huo wakiimba ‘Uhuru Must Go’.

Hali ilivyo uwanjani Uhuru Park

Mwandishi wetu David Wafula yupo uwanja wa Uhuru Park ambapo upinzani umepanga kumuapisha Raila Odinga kuwa kiongozi wa Kenya baadaye leo.

Wafuasi wa upinzani waliozuiliwa Voi waachiliwa

Wafuasi wa upinzani waliokuwa wanasafiri kuelekea Nairobi ambao walizuiliwa awali mjini Voi wameachiliwa na kuruhusiwa kuendelea na safari.

Vituo vya habari vyafungiwa matangazo Kenya

Baadhi ya vituo vya redio na televisheni vya Royal Media Services (RMS), vikiwemo runinga ya Citizen TV, vimefungiwa matangazo pamoja na kituo cha televisheni cha NTV kinachomilikiwa na kampuni ya Nation Media Group (NMG) katika baadhi ya maeneo.

Vituo hivyo vimekuwa vikipeperusha matangazo kuhusu sherehe iliyopangiwa kufanyika leo ya kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga.

Serikali ilikuwa imetahadharisha vituo vya habari Kenya dhidi ya kupeperusha moja kwa moja hafla hiyo.

Mmoja wa wahariri wakuu wa Citizen Peter Opondo ameambia BBC kwamba maafisa wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya (CA) kwamba polisi wakiandamana na polisi walivamia vituo vya kupeperushia matangazo na kuzima matangazo.

Citizen TV ndicho kituo cha runinga kinachoongoza Kenya. Matangazo ya kituo cha NTV yanapatikana pekee kupitia ving’amuzi vya kulipia.

Kituo kingine kikubwa KTN bado kinarusha matangazo.

Fomu 34A na 34B za matokeo vituoni na katika ngazi ya maeneo bunge zilikuwa na utata wakati wa uchaguzi. Mwanamume huyu akaamua kujipamba na 34A na 34B. Na ana ujumbe pia wa Canan Direct – kuashiria matumaini ya kwenda nchi ya ahadi.

Kwa Picha: Wafuasi wa upinzani na mbwembwe zao

Wafuasi wa upinzani wanaendelea kuingia uwanja wa Uhuru Park, baadhi wakiwa wamevalia mavazi yenye ujumbe. Wengine wamevalia kuonyesha uzalendo na wengine utiifu wao kwa Bw Odinga.

Tazama hali ilivyo kupitia picha hizi za waandishi wetu David Wafula na Peter Njoroge.

Maandalizi kwenye jukwaa yaanza Uhuru Park

Maandalizi kwenye jukwaa kuu uwanja wa Uhuru Park yameanza, na viti vimeanza kupangwa.

Gavana wa Mombasa aelekea Uhuru Park

Gavana wa Mombasa Hassan Joho, mmoja wa viongozi wa chama cha ODM chake Bw Odinga, ni miongoni mwa viongozi ambao wamefunga safari kuelekea uwanja wa Uhuru Park.

Kupitia Twitter, amesema ameandamana na viongozi wengine wa kaunti hiyo ya pwani.

Odinga: Kufungwa kwa vyombo vya habari inasikitisha

Raila Odinga azungumza na vyombo vya habari dakika chache kabla ya kuelekea ‘kuapishwa’.

Akizngumza kwa njia ya simu na kituo cha habari cha KTN, Odinga amesema kuwa hawakutarajia kufungwa kwa vyombo vya habari.

Ni hali ya ‘kusikitisha’ na ‘inaonesha kuwa tumefika kiwango cha Uganda.’

Alipoulizwa nani haswa atamuapisha, Odinga alijibu ‘ngoja uone.’

Alielezea kuwa shughuli yao ni halali na haikiuki katiba. Pia amesema haamini kwamba wanachokifanya ni mapinduzi ya serikali.

Odinga: Tunachokifanya si mapinduzi ya serikali

Bw Raila Odinga amezungumza na kituo cha habari cha KTN kwa njia ya simu ambapo amesisitiza kwamba Rais Uhuru Kenyatta hakuchaguliwa kwa njia halali.

Alipoulizwa anni atamwapisha, amesema: “Ngoja uone” na akasisitiza kwamba wanachokifanya leo kina msingi wake katika sheria na si mapinduzi.

“Hatutambui uchaguzi wa Oktoba 26 (uchaguzi wa marudio ambao Odinga alisusia), zaidi ya asilimia 86 ya Wakenya hawakushiriki. Tuna serikali ambayo si halali ambao inajidai kuwa mamlakani,” amesema.

Kuhusu taarifa kwamba amepokonywa walinzi, amesema: “Walinzi wangu waliondolewa muda mrefu sana uliopita. Najihisi kuwa hatarini ndio lakini watu raia ndio usalama wangu.”

Bw Odinga ameitaka serikali kutotumia nguvu kuusambaratisha mkutano wa leo.

“Wafuasi wangu wamo safarini kuelekea Canaan. Safari yetu ni halisi na haiwezi kuzuiwa.

Global Publishers App imekurahisishia kutazama matokeo ya kidato cha nne kupitia simu ya mkononi. Install Global Publishers sasa uyasome yote: Bofya  au 

Comments are closed.