The House of Favourite Newspapers

Live Updates: Maelfu Wajitokeza Kushuhudia Kuapishwa Kwa Uhuru Kenyatta (Video)

0

 

Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

RAIS mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta (56) na Naibu Rais mteule, William Ruto (50) wanatarajiwa kuapishwa leo, kuanza ngwe ya pili ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne.

 

Mkuu wa Utumishi wa Umma, Joseph Kinyua alisema Kenyatta ataapishwa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Michezo Moi, Kasarani jijini Nairobi, kuanzia saa nne asubuhi. Leo ni siku ya mapumziko nchini Kenya.

 

Kiapo hicho kitaongozwa na Msajili Mkuu wa Mahakama, Anne Amadi na kushuhudiwa na Jaji Mkuu wa Kenya, David Maraga. Sherehe hizo zinazotarajiwa kuhudhuriwa na wageni 100,000 wa ndani na nje ya Kenya, zitagharimu shilingi milioni 300 za Kenya (zaidi ya Sh bilioni 6.3 za Tanzania).

Mama Ngina Kenyatta, mamake rais Uhuru Kenyatta.

RAIS mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta (56) na Naibu Rais mteule, William Ruto (50) wanatarajiwa kuapishwa leo, kuanza ngwe ya pili ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Mkuu wa Utumishi wa Umma, Joseph Kinyua alisema Kenyatta ataapishwa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Michezo Moi, Kasarani jijini Nairobi, kuanzia saa nne asubuhi. Leo ni siku ya mapumziko nchini Kenya.

Kiapo hicho kitaongozwa na Msajili Mkuu wa Mahakama, Anne Amadi na kushuhudiwa na Jaji Mkuu wa Kenya, David Maraga. Sherehe hizo zinazotarajiwa kuhudhuriwa na wageni 100,000 wa ndani na nje ya Kenya, zitagharimu shilingi milioni 300 za Kenya (zaidi ya Sh bilioni 6.3 za Tanzania).

Baada ya kiapo, jeshi litapiga mizinga 21 kumkaribisha Rais mpya. Kenyatta amemwalika mpinzani wake mkuu kwenye uchaguzi uliopita, kiongozi wa Muungano wa Vyama vya Upinzani (NASA), Raila Odinga ahudhurie sherehe hiyo.

“Wagombea wengine saba na wagombea wenza wao kwenye uchaguzi uliopita wa Rais wamealikwa kwenye sherehe,” alisema Kinyua. Alitoa mwito kwa wapinzani kusitisha mpango wa kumwapisha Odinga leo na badala yake washirikiane na Serikali kwenye mambo yenye manufaa kwa Wakenya.

Kenyatta aliahidi kuwa Rais wa Wakenya wote, hata ambao hawakumpigia kura Oktoba 26 na hatambagua au kumwadhibu yeyote kwa sababu za msimamo wake wa kisiasa.

Alitaja vipaumbele vyake kuwa kwanza ni amani kwa Wakenya wote, na pili kuhakikisha umoja wa Wakenya wote unakuwa msingi wa kupata maendeleo wanayoyataka. Alitoa mwito kwa viongozi kuweka kando tofauti zao za kisiasa na wafanye kazi pamoja kuboresha maisha ya Wakenya.

Juzi (Jumapili) Kenyatta alihudhuria ibada ya shukurani kwenye Kanisa la Injili la Redeem Huruma, ambapo alisema sherehe za kuapishwa kwenye Uwanja wa Kasarani, hazitakuwa kwa ajili yake kufurahia ushindi, ni za Wakenya kusheherekea amani na umoja wao.

 

Alisema, kwa kuwa Kenya ni nchi ya kidemokrasia, ni kawaida kushindania madaraka ya kisiasa, lakini ushindani huo usiwe kwenye misingi ya ukabila au eneo anapotoka mtu, ila mawazo yatakayoboresha maisha ya Wakenya.

 

“Kama ilivyo kwenye ushindani wowote, kuna washindi na walioshindwa, lakini kwenye uchaguzi sisi wote ni washindi kama Wakenya. Baada ya ushindani wa kisiasa wajibu wetu ni kuungana kuijenga nchi,” alisema Kenyatta.

“Kwenye siasa ni kawaida kuwa na tofauti za kisiasa, lakini hilo halimaanishi kwamba hatuwezi kuwa pamoja na kuishi pamoja kwa amani,” alisema. Kwenye ibada hiyo, Kenyatta na Naibu wake, Ruto walipiga magoti pamoja, wakawekewa mikono kichwani kuombewa.

 

Ruto alisema alikuwa kanisani hapo na Kenyatta kutekeleza ahadi yao kwa Mungu kwamba kama angewapa ushindi watamtukuza. Alitoa mwito kwa viongozi kuweka kando tofauti zao za kisiasa na wafanye kazi pamoja kuboresha maisha ya Wakenya.

 

Msemaji wa Serikali ya Kenya, Erick Kiraithe alisema wakuu 20 wa nchi, wamethibitisha kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Kenyatta, akiwemo Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli ambaye ni kipenzi cha wengi ndani na nje ya Afrika Mashariki.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu pia anatarajiwa kuwa miongoni mwa watakaoshuhudia Kenyatta akiapa. Anatarajiwa kufika Kenya leo asubuhi na ataondoka mara baada ya sherehe za kiapo.

 

Kenyatta na Ruto wanaapishwa kwa kuwa Novemba 20 mwaka huu, Mahakama ya Juu nchini Kenya ilitoa hukumu kwamba ushindi wao kwenye uchaguzi wa marudio Oktoba 26 ulikuwa halali.

 

Kenyatta na Ruto waligombea kupitia chama cha Jubilee kilichoanzishwa Septemba 8 mwaka jana, kwa kuunganisha viongozi wakuu wa Muungano wa Jubilee, The National Alliance (TNA), United Republican Party (URP), na vyama vingine 10 vya siasa.

 

Kwa mara ya kwanza, Kenyatta na Ruto waliapishwa kuongoza Serikali ya Awamu ya Nne baada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika Aprili 2013 kwenye kaunti zote 47 na diaspora. Uchaguzi mwingine utafanyika mwaka 2022 kupata viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.

 

Kwa mujibu wa Kenyatta, Ruto atagombea urais. USHINDI WAKE Anaapishwa kwa kuwa Novemba 20 mwaka huu, Mahakama ya Juu nchini Kenya, iliidhinisha ushindi aliopata wakati wa uchaguzi wa Oktoba 26 mwaka huu.

 

Jaji Mkuu wa nchi hiyo, David Maraga alitangaza uamuzi huo wakati akisoma hukumu ya majaji sita. Awali, Oktoba 30 mwaka huu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC), ilimtangaza Kenyatta kuwa mshindi kwa kupata asilimia 98.26 ya kura zilizopigwa.

 

Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alisema katika uchaguzi wa marudio, Kenyatta alipata kura 7,483,895 kati ya kura halali 7,616,217 zilizopigwa kwenye majimbo 266 kati ya 291. Kwa mujibu wa Chebukati, asilimia 38.84 ya Wakenya 19, 611,423 waliojiandikisha, walipiga kura uchaguzi huo wa marudio.

 

Kura 37,713 ziliharibika. Awali IEBC ilimtangaza Kenyatta kuwa mshindi wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Agosti 8, lakini Septemba Mosi Mahakama ya Juu Kenya ilibatilisha ushindi huo kwa maelezo kuwa taratibu zilikiukwa.

Oktoba 26 mwaka huu, Wakenya walipiga kura na IEBC kupitia kwa Chebukati ikatoa tangazo namba 10808 gazetini, kumtangaza Kenyatta na mgombea mwenza wake, Ruto kuwa ni washindi.

 

 

Kulikuwa na wagombea wanane akiwemo kiongozi wa Muungano wa Vyama vya Upinzani (NASA), Raila Odinga, Ekuru Aukot wa chama cha Third Way Alliance, Cyrus Jirongo (United Democratic Party), Abduba Dida (Alliance for Real Change), na wagombea binafsi Michael Wainaina, Joseph Nyaga na Japheth Kavinga.

 

WASIFU WA KENYATTA Uhuru Kenyatta ni mtoto wa Baba wa Taifa wa Kenya, Rais wa kwanza wa Jamhuri huru ya Watu wa Kenya, Jomo Kenyatta. Uhuru alizaliwa Oktoba 26, 1961. Alisoma Shule ya Mtakatifu Maria jijini Nairobi.

Baada ya hapo, alisoma sayansi ya siasa na uchumi kwenye Chuo cha Amherst, Massachusetts nchini Marekani. Baada ya kuhitimu alirudi Kenya akaanzisha kampuni iliyoitwa Wilham Kenya Limited, iliyonunua na kuuza nje mazao ya kilimo.

Mwanzoni mwa miaka ya 1990, aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Kenya na mwaka 2001 aliteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Kenya, na pia Rais Daniel Arap Moi akamteua kuwa Waziri wa Serikali za Mitaa. Mwaka 2002 Kenyatta aligombea urais kupitia chama cha KANU, akabwagwa na mgombea wa upinzani, Mwai Kibaki.

 

Baada ya uchaguzi huo alichaguliwa kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni. Desemba mwaka 2007 Kenyatta alimuunga mkono Kibaki kwenye uchaguzi wa Rais, na Januari mwaka 2008 aliteuliwa kuwa Waziri wa Serikali za Mitaa. Aprili mwaka 2008 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Biashara kwenye serikali ya mseto.

 

Tangu mwaka 2009 hadi 2012 mwanasiasa huyo alikuwa Waziri wa Fedha na pia akaendelea na majukumu ya Naibu Waziri Mkuu. Kenyatta ana mke, Margaret, walifunga ndoa mwaka 1989, na wana watoto watatu, Jomo Kenyatta, Jaba Kenyatta na Ngina Kenyatta.

 

Wakati huo huo, Serikali ya Kenya imesema kuwa tayari wakuu wa nchi 11 za Afrika, wamethibitisha kushiriki katika sherehe za kuapishwa kwa Kenyatta, huku nchi nyingine 13 zikitarajiwa kuwakilishwa ama na makamu wao, mawaziri au ujumbe maalumu.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya, mbali ya Netanyahu na Rais Magufuli, wengine waliothibitisha na nchi zao kwenye mabano ni Yoweri Museveni (Uganda), Paul Kagame (Rwanda), Ian Khama (Botswana), Edgar Lungu (Zambia), Ismail Omar Guelleh (Djibouti), Hage Geingob (Namibia), Faure Gnassingbe (Togo), Mohamed Farmajo (Somalia) na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn.

 

Nchi zitakazotuma wawakilishi na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ni Nigeria, Guinea, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Burundi na Yemen. Senegal, China na Japan zitatuma ujumbe maalumu wakati Afrika Kusini, Uingereza, Ukraine na India zitatuma mawaziri.

 

Wakati akiapishwa kuwa Rais wa Kenya kwa mara ya kwanza mwaka 2013, wakuu wa nchi 12 walihudhuria. Katika hatua nyingine, Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta sasa anaitwa babu. Amepata mjukuu wa kike aliyepewa jina Wanjiru.

 

Wanjiru ni jina la katikati la mke wa Kenyatta, Margaret. Mjukuu wa mwanasiasa huyo alizaliwa juzi Jumapili kwenye Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Kichanga Wanjiru ni cha mtoto wa kwanza wa Rais Kenyatta, Jomo Kenyatta. Jomo ni jina la baba mzazi wa Rais Kenyatta.

Zambian President H.E. Edgar Lungu has arrived in Nairobi this evening for the inauguration of his Kenyan counterpart President Uhuru Kenyatta and his Deputy William Ruto tomorrow in Kasarani. pic.twitter.com/Y8ylc5n0l6

— AMB:Amina Mohamed (@AMB_A_Mohammed) November 27, 2017

Uganda President Yoweri Kaguta Museveni at Jomo Kenyatta International Airport on arrival this evening to attend President Uhuru Kenyatta inauguration scheduled for Kasarani tomorrow. Also at hand to receive him was Baringo Senator Gideon Moi. pic.twitter.com/6zYQwcldzV

— AMB:Amina Mohamed (@AMB_A_Mohammed) November 27, 2017

Receiving Ethiopian Prime Minister H.E. Hailemariam Desalegn at Jomo Kenyatta International Airport, on arrival for inauguration tomorrow of President Uhuru Kenyatta and Deputy President William Ruto. pic.twitter.com/gAhnwRvthv

— AMB:Amina Mohamed (@AMB_A_Mohammed) November 27, 2017

UPDATES: Msajili Mkuu wa Mahakama, Anne Amadi amemwapisha Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Kenya kwa mhula wa miaka mingine mitano ijayo.

Leave A Reply