The House of Favourite Newspapers

FT: YANGA 0-1 SIMBA KUTOKA UWANJA WA TAIFA

 

FULL TIME

Yanga wanapambana kuwahimiza Simba wache lakini nao hawana haraka.

Simba wanamtoa Kagera na nafasi yake inachukuliwa na Niyonzima.

Ndani ya dakika 4 za nyongeza, Simba wanaonekana kupunguza kasi na Yanga sasa wanajaribu kushambulia kupata bao la kusawazisha.

Dakika za lala salama, Yanga wakumungiza Matheo Anthony badala ya Gadiel Michael na Simba wanamtoa Okwi na nafasi yake inachukuliwa na Muzamiru Yassin.

 

GOOOOOO

Pasi nzuri ya Bocco, Kagere anaunganisha kwa kichwa katika dakika ya 71 sasa Simba wanaongoza

Yanga wamemtoa nahodha Ibrahim Ajibu na nafasi yake imechukuliwa na Mohamed Banka

Yanga wamemtoa nahodha Ibrahim Ajibu na nafasi yake imechukuliwa na Mohamed Banka

Mashambulizi yamekuwa ya zamu, Simba wakishambulia zaidi. Okwi amepiga mpira ukagonga mwamba na mara moja Makambo nusura afunge tena.

Kipindi cha pili kimeanza kwa Yanga kumtoa Amissi Tambwe na nafasi yake kuchukuliwa na Mrisho Ngassa, Simba wametoa Chama na nafasi yake inakwenda kwa Hassan Dilunga.

MAPUMZIKO:
Sasa ni mapumziko mechi ya watani, Yanga wakiwakaribisha Simba.

YANGA:
Mwanzo walianza kulinda, wakiweka wachezaji hadi tisa nyuma ya mpira na kuwapa Simba wakati mgumu sana.

Baada ya dakika ya 25, walianza kubadilika taratibu na kucheza kwa kasi huku Godi, beki wa kulia wa Yanga akiisumbua ngombe ya Simba hadi Zimbwe akalambwa kadi ya njano.

Makambo, mara mbili nusura aifungie Yanga na inaonekana Yanga wamekuwa na nidhamu kubwa katika ulinzi.

SIMBA:
Simba walianza vizuri kipindi cha kwanza wakitawala karibu dakika 20 zote, wakishambulia mfululizo huku Yanga wakimuacha Makambo pekee, mbele.

Hata hivyo, Simba hawakuwa makini kutumia nafasi nyingi walizopata.

Kuanzia dakika ya 28, walianza kuonekana kupoteza kasi waliyonayo na kuwaachia Yanga nafasi kucheza.

PICHA NA MUSA MATEJA, RICHARD BUKOS,  SWEETBERT LUKONGE

Comments are closed.