LIVE: Wagombea Uchaguzi Mkuu wa TFF Mjini Dodoma Wakijinadi

Wagombea Urais, Shija (kushoto) na Mwakalebelea (kulia).

 

MGOMBEA wa nafasi ya Ujumbe ya Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Mazengo kutoka Kanda ya sita (Katavi na Rukwa, amejikuta akishindwa kujibu swali alipopewa nafasi ya kuomba kura.

 

Mgombea Urais, Imani Madega akiwasili.

 

Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unafanyika leo mjini hapa kwenye Ukumbi wa St Gasper kwa ajili ya kuwapata washindi wa nafasi ya urais, makamu wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji.

Masanduku ya kupigia kura yakiandaliwa.

Ilikuwa hivi; Muda wa wagombea kuomba kura kwa mara ya mwisho ulipofika, mgombea Mazembe alipanda jukwaani na kuelezea mikakati yake na alipomaliza mjumbe mmoja akanyosha mkono na kumtaka ataje vyama vya soka vinne vinavyounda Kanda ya Katavi lakini akashindwa na kuibua minong’ono kwa wajumbe wengine.

Na Musa Mateja | Global Publishers |Dodoma

LIVE: Wagombea Uchaguzi Mkuu wa TFF Mjini Dodoma Wanaomba Kura


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Loading...

Toa comment