Majaliwa Azungumza Katika Swala na Baraza la Eid Dar -Video
Eid Al Adha Jijini Dar es Salaam, Majaliwa amesema kuwa ni muhimu kwa wanasiasa kueleza yale waliyopanga kuwasaidia wananchi kuliko kubeza yale yaliyofanywa na wengine na kukashfu.
“Tujiepushe na lugha za uchochezi, tujiepushe na lugha za bezo, tujiepushe na lugha za kashfa kazungumze kile ambacho utawatendea wananchi,” amesema Majaliwa.
Waziri Mkuu pia amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuimarisha amani na mshikamano nchini kwa kutoa mawaidha mazuri yenye lengo la kujenga jambo ambalo limekuwa msaada mkubwa kwa Taifa.
Akielezea kuhusu hayati Benjamini Mkapa ,amesema kuwa waislamu watamkumbuka kwa kuanzisha Chuo Kikuu cha waislamu kwa kutoa majengo ya Serikali na kukabidhi kwa waislamu na hivyo kuanzishwa kwa Chuo Kikuu hicho kilichopo mjini Morogoro.
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8