The House of Favourite Newspapers

Logic; Amewapaisha NANDY, MAUA na Kuambulia Patupu!

0

MUZIKI una nafasi kubwa kwenye maisha yetu ya siku. Muziki umetumika kuleta hamasa kubwa mno ya ufanyaji kazi, kuliwaza baada ya kazi nzito na mengine mengi.

 

Kwa kukuongezea, muziki unaweza kuwa tiba ya maumivu ya moyo.

Kwa kusikiliza tu muziki, mtu anaweza kutoka kwenye msongo wa mawazo ambao ni hatari kwa afya yake.Kwa kulitambua hilo, wanamuziki wameweza kujiongeza na kuimba nyimbo kwa hisia kali, zinazohusu maisha halisi ambayo wengi huyapitia.

 

Wengine wamejikuta wakiweka nguvu zao zote kwenye soko hilo na hatimaye kufanikiwa.Mbali na nyimbo kuimbwa na wasanii, pia wapo watu walio nyuma yao, ambao huwapa kiburi wasanii hao kwa kuwatungia nyimbo nzuri na kukubalika kwenye jamii.

Miongoni mwa watunzi bora Bongo ni Logic, ambaye amewatungia wasanii wengi Bongo akiwemo Nandy, Maua Sama, Malkia Karen, Mwasiti na wengineo.

Tumezungumza naye leo kwenye Mikito Nusunusu, karibu:

MIKITO: Logic mara nyingi Nandy amekuwa akikusifia kwa kumtungia nyimbo nzuri, hivi koneksheni na Nandy uliipata vipi?

LOGIC: Ni kupitia THT.

MIKITO: Ahaa… na wewe ulianzia pale au ilikuwaje?

LOGIC: Ndiyo, nilianzia pale.

 

MIKITO: Ulikuwa pale kama mwanamuziki wa Bongo Fleva au kwenye sekta ipi?

LOGIC: Nilitaka kuwa muimbaji wa Bongo Fleva, lakini baadaye nikawa sina hisia nao tena.

MIKITO: Kipi kilichokufanya hadi kuingia kwenye Gospo, maana tunafahamu unazo nyimbo za Gospo?

LOGIC: Wokovu wangu ulikuja kwa njia tofauti, maana nilijikuta nauchukia muziki wa Bongo Fleva. Nikashangaa nikiimba muziki wa Injili, nafurahia.

MIKITO: Mbali na Nandy, wasanii gani wengine umewahi kuwaandikia?

LOGIC: Malkia Karen, Maua Sama na Mwasiti.MIKITO: Unavyotunga Bongo Fleva na wewe kuimba Gospo, vipi viongozi wa dini hawakupi shida?


LOGIC: Hapana, hawajawahi kuniletea shida kabisa, kwa sababu sifanyi kwa ubaya.

MIKITO: Ikitokea wasanii uliowatungia wakataka kukushirikisha, upo tayari?

LOGIC: Hapana, napenda tu kuwaandikia, na si kushirikiana nao.MIKITO: Kuna mkataba wa kuwaandikia au unajitolea tu?

LOGIC: Sijawahi kupata chochote tangu nimeanza kuandika, wengi hawatimizi ahadi zao. MIKITO: Yaani wanakuahidi halafu hawakulipi?

LOGIC: Sio wa kweli kwa kifupi, lakini tunapambana.

MIKITO: Pole sana. Kipi kinakusukuma kwenye utunzi wako?

LOGIC: Kinachonisukuma, watu wengi wanajifunza kupitia mimi, sasa naogopa kuwavunja moyo. Inanibidi nipambane nifi ke, japo napitia magumu mengi.

MIKITO: Idea za nyimbo unazitoaga wapi?

LOGIC: Idea nyingi zinatokana na maisha yangu binafsi na mambo niliyoyaona kupitia kwa ndugu na jamaa zangu.

 

MIKITO: Unapata ugumu gani kumtungia Nandy?

LOGIC: Huwa sipati ugumu, ila nakumbana na changamoto kwa sababu Nandy ni msanii mkubwa. Kwa hiyo, lazima umuandikie nyimbo inayoendana na ukubwa wake, hiyo ndiyo changamoto kubwa kwangu.

 

MIKITO: Ilikuwaje hadi ukajikuta mtunzi mzuri?

LOGIC: Sikuwa naamini kama naweza kutunga, ila marehemu Ruge Mutahaba, ndiye aliyeona uwezo wangu wa kutunga sana kuliko kuimba.

MIKITO: Wimbo wako wa kwanza kuutunga ulikua upi na ulimtungia nani?LOGIC: Unaitwa Sijui, aliuimba Amini wa

 

THT.MIKITO: Mafanikio gani uliyoyapata kutokana na utunzi?

LOGIC: Nimefahamika tu, ila kuhusu mafanikio, kiukweli bado sijayaona.

MIKITO: Changamoto zipi unazopitia?

LOGIC: Changamoto ni nyingi sana, lakini nashindwa kuzieleza.

MIKITO: Vipi kuhusu familia, yaani mke na watoto!LOGIC: Sina mke wala mtoto.

MIKITO: Ndoto zako ni zipi?LOGIC: Kuwa mwimbaji mkubwa wa muziki wa Injili, pia kuweka historia kwa vijana wa Kitanzania waliopitia maisha duni, kuwa waamini katika vipaji vyao na wasiziache ndoto zao njiani. MIKITO: Mbali na sanaa, unajihusisha na nini?


LOGIC: Nafanya sanaa tu, sina kingine.

MIKITO: Una nyimbo ngapi za Gospo hadi sasa?

LOGIC: Zilizotoka ni tatu; Zawadi, Ni kwa Muda na Rafi ki, ingawa zisizotoka nazo ni nyingi sana.MIKITO: Mashabiki wamekupokeaje?

LOGIC: Namshukuru Mungu, nimepata mrejesho mzuri.

MIKITO: Una kipi cha kuwaambia mashabiki zako?

LOGIC: Sina cha kuwaambia zaidi ya kusema nashukuru kwa mapokezi yao makubwa, kikubwa naomba waendelee kunisapoti.

MAKALA: AMINA SAID, RISASI

HALI MBAYA! DC SABAYA Akuta WANAFUNZI WAKIUME Wanalala KITANDA KIMOJA, Atoa MASAA 24 kwa MMILIKI…

Leave A Reply