The House of Favourite Newspapers

Lori la Mafuta Laanguka Kagera, Wanane Mbaroni Wakiiba Mafuta

WAKATI bado Watanzania wakiendelea kuomboleza vifo vya watu 102 kufuatia ajali ya moto wa ya lori la mafuta iliyotokea mjini Morogoro, baadhi ya wananchi wa Kagera wamejitokeza kwa wingi kuchukua mafuta lori la mafuta lililoanguka jana eneo la Benako, Ngara, mkoani Kagera.

 

Katika na tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani humo limewakamata watu wanane kwa tuhuma za wizi wa mafuta kutoka gari hilo.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi, amesema pia wamekamata lita 300 za mafuta, zilizoibiwa kwenye ajali hiyo.

Comments are closed.