The House of Favourite Newspapers

Lubuva: Wananchi msihofu uchaguzi utakuwa wa amani

0

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva (katikati) akiwa na makamishna wa tume hiyo wakati akisisitiza jambo kwenye mkutano wake na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.

Makamishna wa Tume hiyo wakiwa bize kwenye mkutano huo.

Jaji mstaafu John Mkwawa (kushoto) akiandika mambo yaliyokuwa yakiendelea wakati wa mkutano huo.Kaimu Mkurugenzi wa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Giveness Aswile akiwa makini kusikiliza yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.
Moja wa wahariri akimuuliza swali mwenyeti wa tume, Jaji Lubuva kuhusiana na mchakato wa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25.

Mhariri Mkuu wa Gazeti la Uwazi Mizengwe, Daniel Mbega akitoa ushauri wa kiusalama kwenye mkutano huo kuhusu masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu ambapo Jaji Lubuva alimshukuru na kusema ameupokea.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewatoa wasiwasi wananchi kwamba uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na rais unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu utakuwa wa amani.

Lubuva alitoa kauli hiyo leo katika mkutano baina ya tume hiyo na wahariri wa vyombo mbalimbali ambao umefanyika kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.Akizungumza huku akiwa sambamba na makamishna wa tume hiyo, Lubuva alisema tume yake imejiandaa vizuri kwa uchaguzi huo.

“Mtu au chama chochote kisihofu kuhusu uchaguzi kwani utakuwa wa amani na utulivu kwa nchi nzima, kwani imeweka mazingira mazuri kwa wananchi kupiga kura bila tatizo,” alisema Lubuva.

Aidha, mwenyekiti huyo ametoa rai kwa wananchi mara wakimaliza zoezi la kupiga kura warudi majumbani mwao kusubiri matokeo kutangazwa na mamlaka husika.

(HARUNI SANCHAWA WA GPL)

 

Leave A Reply