The House of Favourite Newspapers

Lugola: ‘Siwezi Kurudia’

0

IKIWA ni siku mbili baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, kuenguliwa kwenye wadhifa wake na Rais  John Magufuli, Mbunge huyo wa Mwibara, Bunda mkoani Mara amefunguka na kusema haya:

 

“Siwezi kurudia; Mheshimiwa rais alizungumza na Watanzania pale kwa hiyo mimi sioni sababu ya mimi kurudia tena. Naomba Watanzania waendelee kumuamini rais, kumuunga mkono katika juhudi za serikali na sisi tutaendelea kumuunga mkono.

 

“Kwa hiyo mimi niko vizuri na wala msidhani kuwa kuna shida imenitokea katika hatua hizo. Ni hatua nzuri, njema kabisa naomba muelewe hivyo na kuendelea kuchapa kazi.

 

“Sisi wabunge wa CCM wakichukuliwa wachache kuunda baraza, na sisi tunakuwa benchi; ni wachezaji wakati wote, tunapiga jaramba tunaweza kuingia na sisi.

 

“Sasa ambao tuko benchi tunaendelea kuwashangilia waendelee kumsaidia rais hadi watakapomaliza awamu na kuingia kwenye uchaguzi.”

 

Leave A Reply