The House of Favourite Newspapers

Lukamba Afunguka Usiyoyajua Kwa Diamond Platnumz -Video

Mpiga picha na mwongozaji wa video za Wasafi, Lukamba (kushoto),  akifanya mahojiano na Global TV Online.

 

MPIGAPICHA na mwongozaji wa video za Diamond na Wasafi, Lukamba,  amefanya mahojiano na Global TV Online  baada ya kuzawadiwa gari mpya aina ya Toyota Alteeza na msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

 

Katika mahojiano hayo Lukamba amesema amekuwa akitumiwa meseji nyingi kupitia Insta Dm, huku wakimmwagia sifa mbalimbali, Pia amefunguka kuwa gari aliyopewa na bosi wake hakatwi chochote kwenye mshahara wake.

“Lukamba anakaa Bunju, kuna kipindi alikabwa na kuchukuliwa hadi laptop sasa leo nampatia gari,” aliyasema Diamond Platnumz akiwa katika tafrija aliy­oifanya mitaa ya Tandale-Sokoni katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo aligawa misaada mbalimbali kwa wananchi wa Tandale.

TAZAMA MAHOJIANO YA LUKAMBA NA GLOBAL TV HAPA CHINI

Comments are closed.