The House of Favourite Newspapers

Lulu Arudi Kwa Kishindo Instagram na Mahaba kwa Majizzo

Mwigizaji wa filamu maarufu Bongo, Elizabeth Michael.  

Mwigizaji wa filamu maarufu Bongo, Elizabeth Michael hatimaye leo amerudi rasmi kwa kishindo kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram kwa kuposti ujumbe wa mahaba kwenda kwa mpenzi wake Majizzo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha Redio cha EFM na Kituo cha Televisheni cha TV-E.

Lulu aliandika ujumbe uliosomeka “Lover,Best Friend,Business Partner,Ride Or Die And A Shoulder To Always Cry On. Asante Kwa Kunionyesha Maana Halisi Ya Upendo Wa Agape(KIUNGU). Baraka Zikufuate Siku Zote Za Maisha Yako.” .

Tangu mwanadada huyu ahukumiwa kwenda jela mwaka jana kwa kosa la kuua bila kukusudia na hata, baadaye alipotolewa jela kwa msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli, Lulu alikuwa hajaposti lolote lile mpaka leo hii.

Baada ya kuposti ujumbe huo ambapo leo ni siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake  Majizzo, mashabiki wake wengi walionyesha  kufurahishwa zaidi na kitendo hicho kwa kuishambulia posti hiyo na komenti za kumkaribisha mitandaoni.

 

Comments are closed.