Lulu Atoa Kali Ya Mobeto

Staa machachari wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa kali kuwa, kama ni kweli watoto wa mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto wanafafana naye, basi mimba za mwanamama huyo huwa zinampenda.

Lulu amesema hayo baada ya shabiki mmoja kwenye Mtandao wa Instagram kuposti picha ya Lulu, Hamisa na watoto wake na kumuuliza kwa nini watoto wake wanafanana na yeye kuliko mama yao?

 

Lulu alitoa jibu kuwa, mimba za mama yao huwa zinampenda yeye.

“Ndiyo. Ninafanana nao kwa sababu mimba za Hamisa zinanipendaga sana,” aliandika Lulu.

 

Jibu hilo liliwaacha mdomo wazi mashabiki wake huku wengine wakiwa na maswali kibao vichwani mwao, wakijiuliza kwa nini staa huyo anawajibu shiti mashabiki.

Toa comment