The House of Favourite Newspapers

LULU AWEKEWA ULINZI MZITO

Elizabeth Michael ‘Lulu’

BAADA ya kuvishwa pete ya uchumba na mipango ya harusi ikielezwa kushika kasi, mrembo wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewekewa ulinzi mzito kuhakikisha hakuna mtu anamsogelea hovyo.

 

Awali, Amani lilielezwa kuwa, tangu Lulu avalishwe pete ya uchumba na kuwa mke mtarajiwa, aliwekewa ulinzi huo binafsi hivyo kila anapokuwa, lazima awe na bodigadi. Nafikiri jamaa wake kaona ni vizuri kwa vile Lulu ni staa na kumtengenezea muonekano wa kistaa, ni vizuri akawa na mlinzi binafsi, sasa hivi ana bodigadi anaitwa Livingstone,” kilieleza chanzo.

 

Baada ya kutonywa hilo, Amani lilijiridhisha wikiendi iliyopita maeneo ya Makumbusho kwenye jengo la LAPF baada ya kumnasa msanii huyo akiwa na bodigadi huyo mwenye ‘miraba minne’ alipokuwa amehudhuria kwenye harusi ya jamaa anayefahamika kwa jina la Renatus Nyakai na mkewe Glorian Jarimo.

 

Mwandishi wa Amani ambaye alikuwa mmoja wa waalikwa katika harusi hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa na mkewe, alimfuatilia Lulu mwanzo mwisho tangu anaingia ukumbini.

 

Watu wakiwa tayari wameshaingia ndani ya ukumbi, ilipofika saa mbili na nusu usiku Lulu aliingia ukumbini hapo akiwa na mlinzi wake huyo ambaye alionekana kuwa makini na kazi yake. Lulu alielekezwa sehemu yake ya kukaa huku bodigadi huyo akisimama jirani yake kuhakikisha hakuna mtu anayemsogelea bila ruhusa maalum kuanzia mwanzo hadi mwisho wa shughuli.

Aidha, mshereheshaji wa shughuli hiyo, mtangazaji Gardner Habash mara baada ya utambulisho wa ndugu wa wenye shughuli alimuomba Lulu kufika mbele japo kuwasalimia watu na kutoa mkono wa pongezi kwa bibi na bwana harusi.

 

Mmoja wa shabiki wa Lulu aliyejitambulisha kwa jina la Lucy Mnyate aliyeshuhudia jinsi Lulu alivyokuwa akilindwa, alipongeza na kusema anastahili kwani ni staa mkubwa.

“Unajuwa Lulu ni kipenzi cha watu sana na zamani hatukuwa tumezoea hivyo ilikuwa kila akionekana watu tunajifotolesha mapicha lakini kwa sasa haya nafikiri ni mabadiliko mazuri kwani ni staa mkubwa,” alisema shabiki huyo.

 

Jitihada za kumpata Lulu ukumbini humo ili aongee chochote hazikuzaa matunda kutokana na mlinzi huyo kutoruhusu Lulu afanyiwe mahojiano. Hata hivyo, Amani lilielezwa na mtu wa karibu wa Lulu kuwa mlinzi huyo maalum aliyekuwa naye, amekuwa pia akimlinda mume mtarajiwa sehemu mbalimbali

Stori: Mwandishi Wetu, Amani

Comments are closed.