The House of Favourite Newspapers

Lulu Diva Aibuka na Kufuru Ya Fedha

0

MSANII wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefanya kufuru ya fedha baada ya kufungua saluni ya kike ya kisasa inayoenda sambamba na kuuza vipodozi vya aina mbalimbali, Mikocheni Jijini Dar.

Hatua hiyo ya Lulu Diva ambaye hivi karibuni ameachia ngoma kali ya ‘Hauna maajabu’, imeonekana wazi kufuata nyayo za mastaa wenzake Nandy na Tunda.

 

Akizungumza na RISASI, Lulu alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu anaona kutegemea kitu kimoja kama chanzo cha kumuingiza pesa sio jambo la busara.“Nimeona ni bora kuhangaika kufanya vitu vingine vya kuniingiza kipato.

Na lengo langu lilikuwa ni kufanya biashara ya kitu kizuri ambacho kitapendwa na wanawake wenzangu.“Unajua kwanza mimi mwenyewe napenda sana mambo ya urembo siwezi kwenda sehemu bila kufanya ‘makeup’, hivyo nimeona ni afadhali nifungue saluni.“

 

Ndio maana nimeona nitengeneze kitu kizuri na sio feki ili wanawake wezangu wapendeze na vitu vyenye ubora na sio vya kuwaharibu kuanzia nywele mpaka ngozi” alisema Lulu.

 

Mrembo huyo aliongeza kuwa ndoto hiyo alikuwa nayo kwa kipindi kirefu lakini alikuwa hajui njia gani ataifanya ili aweze kuianzisha.

 

“Kweli kila kitu ni hatua na dua kwa sababu hii ni ndoto yangu ya miaka mitano iliyopita, lakini nashukuru sasa nimefanikiwa na nimewekeza fedha nyingi ili niwapatie wateja wangu vitu vizuri.

 

“Mimi mwenyewe kijiwe changu kitakuwa hapa Mikocheni, nitawahudumia wateja mwenyewe,” alisema Lulu Diva’ ambaye inakadiriwa kutumia zaidi ya milioni 30 kukamilisha mradi huo.

MAKALA:MEMORISE RICHARD, Risasi

Leave A Reply