Lulu diva ataja siri kuvaa nusu utupu

KUTOKANA na hivi karibuni kuonekana kucharuka kwa kuvaa nusu utupu, staa wa muziki wa Bongo Fleva; Lulu Abasi ‘Lulu Diva’ ameibuka na kuanika siri inayomfanya kuwa hivyo.  Akichonga na Amani, Lulu Diva alisema siri ya kuvaa nusu utupu ni kwamba anapenda sana kwa kuwa nguo hizo zinamfanya awe huru kila anakokwenda hata mbele za watu anakuwa jasiri zaidi.

“Napenda sana kuvaa nguo fupi zinazoonesha jinsi nilivyoumbika kwa kuwa nakuwa huru zaidi, sijali mtu mwingine ataizungumziaje maana watu wamezoea kutoa povu kwa kila kitu kiwe kibaya au kizuri kwa hiyo sijali wala nini, nitaendelea kuvaa ninachokipenda ili mradi niwe huru,” alisema Lulu Diva

 

Stori: Neema Adrian, Amani

Toa comment