The House of Favourite Newspapers

LULU DIVA AWEKA WAZI KILICHOBADILI MAISHA YAKE

Picha inayohusiana
Lulu Abass ‘Lulu Diva’

MWANADADA Lulu Abass ‘Lulu Diva’ amebonga kwamba miongoni mwa vitu vilivyombadilisha maisha yake hasa kwenye gemu la Muziki ni wimbo wake wa Ona aliomshirikisha Rich Mavoko.

Akichezesha taya na Star Showbiz, Lulu Diva alieleza kwamba nyimbo zake za nyuma zilikuwa ni nzuri na zilifanya vizuri lakini baada ya Wimbo wa Ona, umemfanya atambulike kwenye gemu la Bongo Fleva kama msanii mkubwa na kumpatia shoo za kila mara.

“Wimbo wa Ona umenipeleka kwenye levo nyingine kabisa kiukweli. Kwa sasa na mimi ni miongoni mwa wasanii wakubwa, shoo zimeongezeka na hata hadhi pia,” alisema Lulu Diva.

Comments are closed.