The House of Favourite Newspapers

Kangi Lugola Amsweka lupango Askari Polisi – Video

ASKARI Polisi mmoja wa Kituo cha Utalii na Diplomasia Mjini Arusha, jana alijikuta akizindua mahabusu ya kituo hicho kwa kuwekwa mahabusu kwa agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola.
Kituo hicho kilizinduliwa na Rais John Magufuli mapema mwaka huu ambapo tangu wakati huo hakijawahi kupokea mahabusu yeyote. Waziri Lugola, ametoa agizo hilo jana Jumatatu, Julai 23 alipotembelea kituo hicho cha kisasa, ambapo akiwa hapo alimuhoji baadhi ya mambo kadhaa ambayo askari huyo alishindwa kuyajibu kwa ufasaha.
“Nimeingia kwenye chumba cha mashtaka, nikamkuta askari nikamuuliza vitabu muhimu kwenye chumba hicho akabaki ameduwaa, nikamuagiza RPC (Kamanda wa Polisi) amuweke ndani. Lakini baadaye nikaamuru atolewe kwani yawezekana askari huyo hana elimu ya masuala ya utalii,” amesema.
Amesema kama kituo hicho hakijawahi kuweka mahabusu mtu, basi askari huyo amekuwa wa kwanza kukifungua kwa kukaa mahabusu,” amesema Waziri Lugola.

BREAKING: LUGOLA Amsweka Selo ASKARI Arusha

Comments are closed.