The House of Favourite Newspapers

LUPITA ANG’ARA UZINDUZI  ‘BLACK PANTHER’ KOREA

Lupita Nyong’o akiwa ameng’aa katika gauni lake siku ya uzinduzi wa Black Panther jijini Seoul, Korea ya Kusini, Jumapili iliyopita.

 

Chadwick Boseman, nyota wa Black Panther, akijulikana kama T’Challa akiwa katika uzinduzi huo.
Lupita akifurahia kinyango cha mfano wake (kulia chini) katika filamu hiyo.
Michael B. Jordan, aliyeigiza adui wa T’Challa, akiwa Korea katika uzinduzi huo.
Lupita akizungumza kwenye hafla hiyo.
…Akipita kwa madaha mbele ya mashabiki.
‘Jopo kuu’ la Black Panther.
T’Challa akisalimia mashabiki.
Lupita akiwa ameachia tabasamu la nguvu.

MCHEZA sinema maarufu wa Kenya, Lupita Nyong’o, mwishoni mwa wiki iliyopita aling’ara katika uzinduzi wa filamu ya Black Panther huko Seoul,  Korea Kusini.

Katika filamu hiyo inayoogozwa na nyota mcheza filamu wa Marekani, Chadwick Boseman, ambaye ndiye Black Panther, akitumia jina la T’Challa, Lupita anacheza kama mkewe aitwaye Nakia.

 

Simulizi ya filamu hiyo inamhusu T’Challa anayerejea nyumbani katika nchi moja ya Afrika iitwayo Wakanda akitokea ughaibuni ambako anakumbana na matatizo kibao katika kuitawala baada ya kurithi ufalme kutoka kwa baba yake.

 

Adui yake ambaye ni Michael B. Jordan anaendesha njama za kumng’oa T’Challa.

 

Matokeo yake uadui huo  unamsababishia matatizo makubwa yanayoenea dunia nzima ambapo Nakia anabidi kufanya kazi ya ziada kuyapeleleza majeshi ya nchi hiyo na kujua siri zake ili kuongeza uimara wa mfalme wa nchi hiyo katika utendaji kazi wake wa kasi, nguvu, uwezo wa kuona gizani na uponyaji.

 

Hata hivyo, mambo yanavyozidi kuvurugika, T’Challa na Nakia wanatengana.

 

Washiriki wengine maarufu katika filamu hiyo ni Danai Gurira, Martin Freeman, Daniel Kaluuya, Letitia Wright, Winston Duke, Angela Bassett, Forest Whiteker na Andy Serkis.

 

Filamu hiyo inategemewa kuonyesha mara ya kwanza Marekani, Februari 18 mwaka huu.

 

Korea Kusini  imepewa fursa hiyo kutokana na baadhi ya matukio muhimu katika filamu hiyo yalifanyika katika nchi hiyo ya bara la Asia, hususan eneo la jiji la Busan ambako hufanyika matamasha makubwa zaidi ya filamu kila mwaka.

 

  1. Lupita Nyong’o akiwa ameng’aa katika gauni lake siku ya uzinduzi wa Black Panther jijini Seoul, Korea ya Kusini, Jumapili iliyopita.
  2. Chadwick Boseman, nyota wa Black Panther, akijulikana kama T’Challa akiwa katika uzinduzi huo.
  3. Lupita akifurahia kinyango cha mfano wake (kulia chini) katika filamu hiyo.
  4. Michael B. Jordan, aliyeigiza adui wa T’Challa, akiwa Korea katika uzinduzi huo.
  5. Msimamizi na mwongozaji wa filamu hiyo, Ryan Coogler, akiwa kwenye uzinduzi.
  6. Lupita akizungumza kwenye hafla hiyo.
  7. …Akipita kwa madaha mbele ya mashabiki.
  8. ‘Jopo kuu’ la Black Panther.
  9. T’Challa akisalimia mashabiki.
  10. Lupita akiwa ameachia tabasamu la nguvu.

 

 

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA YA HABARI

 

 

Comments are closed.