The House of Favourite Newspapers

Luvo Manyonga: Bingwa wa Dunia na Mshindi wa Olimpiki na Vita Yake ya Madawa ya Kulevya

0
Luvo Manyonga Mwanariadha wa Afrika Kusini aliyefungiwa kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya

MWANARIADHA wa mbio za kuruka Luvo Manyonga ambaye ni muathirika wa madawa ya kulevya yaitwayo Tik, hii ni aina ya Crystal Methamphetamine ambayo husagwa na kuwa unga wa chenga huuzwa pande za Afrika Kusini mjini ikiwa kwenye majani ya kukauka, Manyonga alijikuta akipambana na uraibu wa madawa hayo ya kulevya.

 

Manyonga aliweza kujizuia matumizi ya madawa hayo ya kulevya kwa muda mchache ila baada ya mama yake mzazi Luvo kufariki dunia mwaka 2020, hakuweza kujizuia tena mwisho wake akatumbukia katika uraibu wa madawa hayo ya kulevya huku akisema:

 

” Baada ya kumpoteza mama yangu mambo yalienda ndivyo sivyo kwangu mimi, sijui kama unanielewa?”

 

Manyonga alizungumza huku akikumbukia miaka yake miwili iliyopita.

 

Alikuwa akitumia madawa ya kulevya ili apunguze maumivu ambayo alikuwa akihisi kwa ajili ya kifo cha mama yake na hakuweza kufanya maombolezo na alitaka kutumia madawa ya kulevya kutwa kiasi kwamba asikumbuke hata tarehe.

 

Joyce, marehemu mama mzazi wa Manyonga alilea watoto wawili wa kiume ikiwemo Manyonga pamoja na dada yao peke yake kwenye nyumba ndogo yenye vyumba vinne huko Machule Street, karibu na barabara ya vumbi mjini Mbwekeni nchini Afrika Kusini, alifanya kazi kama msafishaji na aligawanya kwa umakini pesa aliyopata kama mshahara kwa wiki 120 Rand na muda mwingine alifanikiwa kupata 5 Rand kwa ajili ya tiketi ya Manyonga ya kwenda Stellenbosch kufanya mafunzo.

Luvo Manyonga

Kifo cha mama yake Luvo kilimuuma kiasi cha kufikia kuiba, kuvamia magari na nyumba, manyonga amesema:

 

” Ningepoteza maisha yangu, nilikuwa nafanya vitu vya kijinga lakini nashukuru mungu alikuwa na mimi na bado nipo hai ”

 

Manyonga amesema aliishawahi kutumia madawa hayo ya kuelevya na akafanikiwa kushinda na kuondoka na dhahabu, akawa ana mawazo kwamba kama alishafanya mara moja na akashinda hashindwi kurudia tena na akafanikiwa lakini alikuwa akijidanganya ilikuwa ni madawa ya kulevya ndio yanamfanya awe na mawazo hayo, manyonga amesema:

 

” Watoto walikuwa wakinifuata kipindi natembea mtaani nimelewa madawa na kuniuliza ‘ Luvo tutakuona lini tena kwenye Televisheni?’ ”

 

Kwa Manyonga maneno kama haya ndiyo yaliyomsukuma kuendeleza mapambano ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya, japo Manyonga alipewa adhabu ya muda kuzidi mwanariadha mwenzie ambae alikutwa ametumia madawa ya kuongeza nguvu mara mbili ambapo kuishia kupewa adhabu ya muda mfupi.

 

Aidha Manyonga ameridhika na kusema kuwa hiyo adhabu ilikuwa ni kumkumbusha inabidi aamke na abadilike, na kwa hivi sasa Manyonga anasubiri baada ya miaka miwili ili kupata nafasi ya kurudi tena kwenye mashindano hayo.

 

Imeandikwa na Arafat Ramadhan Salem kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply