The House of Favourite Newspapers

Lwandamina Amkataa Muivory Coast Azam

0
George Lwandamina

IMETHIBITISHWAkuwa Klabu ya Azam imefikia makubaliano maalum ya kuachana na mshambuliaji wake raia wa Ivory Coast, Richard Djodi kufuatia kocha mkuu wa klabu hiyo, George Lwandamina kumtoa kwenye mipango yake.

 

Djodi amekipiga kwa kipindi cha msimu mmoja pekee ndani ya kikosi cha Klabu ya Azam ambapo alisajiliwa rasmi na kikosi cha Azam akitokea Ashanti Gold ya Ghana Julai 11, mwaka jana.

 

Akizungumza naChampioni Jumamosi, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ alisema ni kweli wameamua kuachana na nyota huyo na hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza mzunguko wa pili.“

 

Ni kweli Klabu ya Azam, imefikia makubaliano ya kuachana na mshambuliaji wetu Richard Djodi, hii ni baada ya kocha Lwandamina kumuondoa kwenye mipango yake hivyo nyota huyo hatakuwa sehemu ya kikosi cha Azam kitakachocheza kwenye michezo ya mzunguko wa pili.

 

“Kuhusu David Mapigano Kissu, yeye bado ataendelea kuwa sehemu ya kikosi chetu kwa kuwa kocha bado anaamini ana msaada, hivyo taaarifa ya kwamba ataachwa hazina ukweli wowote,” alisema Thabith. Azam FC imejichimbia visiwani Zanzibar ambapo watacheza michezo mitatu ya kirafiki kabla ya kurejea Dar Januari 22, mwaka huu

Leave A Reply