The House of Favourite Newspapers

Lwandamina: Kwani wao ni wanyama…

Omar Mdose, Dar es Salaam |  CHAMPIONI JUMAMOSI| Dar es Salaam

MECHI ya watani ina vituko vingi, kwani Kocha wa Yanga, George Lwandamina amesema kikosi chake akimuogopi mchezaji yeyote wa Simba katika mchezo wao wa leo na kuhoji: “Kwani wao wanyama?” Lwandamina raia wa Zambia alikuwa akijibu swali aliloulizwa kuhusu mchezaji anayemuhofia katika kikosi cha Simba anachopambana nacho leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akijibu swali hilo, Lwandamina alisema: “Kwani wao ni wanyama mpaka wawe hatari kwetu? Ninachoweza kusema ni kwamba timu kama timu inaundwa na kila mchezaji. “Ukiona mchezaji amepangwa siku hiyo basi unatakiwa kufahamu kwamba ana umuhimu wake, lakini juhudi zako ndizo zinakufanya uonekane hatari.

“Hivyo siwezi kusema nani tunamuhofia ndani ya Simba, bali tumejipanga kukabiliana na wachezaji wao wote.” Hii ni mara ya kwanza kwa Lwandamina kukutana na Simba katika Ligi Kuu Bara kwani kwa mara ya kwanza alikutana na timu hiyo Januari 11, mwaka huu huko Zanzibar ambapo Yanga ilifungwa kwa penalti 4-2.

Lwandamina ambaye timu yake ni ya pili katika ligi ikiwa na pointi 49 ilizopata katika mechi 21 huku Simba ikiwa nazo 51 katika michezo 22, alisema mchezo wa leo utatoa mwanga wa timu itakayokuwa bingwa msimu huu.

Comments are closed.