The House of Favourite Newspapers

LYNN WA DIAMOND ADAIWA KUBANJUKA NA IDRIS

Irene Geofrey ‘Lynn’

MUUZA nyago kwenye video za Kibongo ambaye hakauki vituko mitandaoni hasa kwenye Mtandao wa Instagram, Irene Geofrey ‘Lynn’, anadaiwa kuwa kwenye mahaba mazito na mchekeshaji Idris Sultan, ambaye ni mshindi wa Shindano la Big Brother 2014.

 

Gumzo juu ya uhusiano wa wawili hao lilianza juzikati ambapo watu wengi walipigia mstari baada ya mwanadada huyo kuposti picha ya Idris huku akiandika maneno ya kimahaba yalisomeka; “Babyboo baby boo bae.”

 

Baada ya kutupia picha hiyo iliyokumbana na komenti nyingi za mashabiki wao wengine wakionyesha kumtakia kheri kwenye uhusiano huo, Risasi Vibes liliamua kumcheki ili kusikia kauli yake ambapo alipopatikana alisema haya;

“Unajua muda mwingine unaweza kuposti kitu halafu maneno yakajiandika yenyewe, sasa ndicho kilichonitokea na mimi sikutaka kufuta kwa sababu watu wangesema ni kiki.

“Lakini Idris ni mshikaji wangu wa karibu sana na ninampenda anavyochekesha, watu wasinitengenezee mambo ambayo hayapo jamani,” alisema Irene.

STORI: SHAMUMA AWADHI

Comments are closed.