The House of Favourite Newspapers

MAAJABU: Mwanamke Azaa Watoto Watano kwa Mpigo

HAYA ni maajabu ya dunia! Hivi ndivyo unavyoweza kusema kufuatia Bi. Honoratha Nakato kutoka Uganda kuandika historia mpya barani Afrika baada ya kujifungua watoto watano mara moja, na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza kusini mwa  Jangwa la Sahara kuzaa idadi hiyo kupitia njia ya IVF (kupandikiza mayai).

 

Akizungumzia furaha yake, Honoratha amesema amekuwa kwenye ndoa kwa miaka 24 lakini hakubahatika kupata mtoto, lakini alipofanya vipimo na kugundua kuwa ana uwezo wa kuzaa kwa njia ya IVF alimshukuru Mungu na sasa ndoto yake ya kulea watoto wake imetimia tena watano kwa mkupuo.

 

Anasema mume alidhani huenda angejifungua hata wawili lakini haikuwa hivyo, baada ya kufika leba na kufanyiwa upasuaji, mtoto wa kwanza alitoka mwanamke, na wa pili lakini wa watatu na wa nne walikuwa wa kiume huku wa tano akiwa wa kike.

 

Mwanamke huyo amesema hakujali gharama kubwa alizokuwa akiambiwa kwa sababu lengo lake ilikuwa ni kupata mtoto. Hata hivyo,  baada ya kujifungua,  mume wake hajafika hospitali siku ya tatu licha ya kupigiwa simu na mkewe baada ya kupata mshituko kutokana na taarifa hizo njema.

 

Bi. Honoratha ana changamoto nyingine ya kunyonyesha kwani mwaka jana alipata saratani ya titi ambapo titi lake moja lilikatwa.

 

CREDIT: AZAM TV

Comments are closed.