MAAJABU: OPRAH ANA MIKONO MITATU, MWIGIZAJI MIGUU MITATU!
JARIDA maarufu nchini Marekani la Vanity Fair linalobeba habari za utamaduni, fasheni na matukio ya sasa na kuchapishwa na kampuni ya Condé Nast, hivi karibuni lilifanya kioja katika kuhariri picha zake kwa ajili ya toleo la 24 la mwaka la ‘Hollywood’ ambapo katika picha ya kwenye jalada lake, mtangazaji maalum wa vipindi vya televisheni, Oprah Winfrey (63), alijikuta akiwa na mikono mitatu, na mcheza sinema Reese Witherspoon (41) alionekana ana miguu mitatu!
Katika picha hiyo, Oprah anaonekana ana mkono mmoja ulioshikakiuno chake, mmoja ukiwa juu ya paja lake na mwingine umezingira kiuno cha Reese. Naye Reese aliye kando ya Oprah, pamoja na kuwa na miguu mwili inayoonekana mbele, anaonekana ana mguu wa tatu unaotokea juu kwenye sketi yake ndefu iliyochanwa pembeni na kuendelea hadi chini pembeni mwa miguu hiyo miwili!
Watu waliuvamia mtandao wa Twitter siku ya Alhamisi na kulikejeli jarida hilo kwa makosa hayo ambapo ilijulikana kwamba kasoro hizo zilitokana na kuondolewa kwa picha ya James Franco kwenye picha hiyo kutokana na madai ya tabia yake mbaya kuhusiana na masuala ya ngono.
(WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA YA HABARI)
Comments are closed.