The House of Favourite Newspapers

Mkude: Kwa Mfaransa Huyu, Tumelamba Dume

KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude, amefunguka kuwa, kufuatia ujio wa kocha mpya katika timu yao hiyo, Pierre Lechantre raia wa Ufaransa ni faraja kwao kuweza kufanya vizuri kwenye ligi na michuano ya kimataifa.

 

Mfaransa wa Simba ametua nchini mapema wiki iliyopita akichukua mikoba ya Mcameroon, Joseph Omog aliyetimuliwa baada ya kutolewa katika michuano ya FA.

Pierre ametua nchini ikiwa ni moja ya ahadi ya bilionea Mohamed Dewji ‘Mo’ ambaye anahitaji kuibadilisha Simba kuwa ya kimataifa kwa kutoangalia ligi ya ndani pekee.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkude alisema kuwa, ujio wa kocha huyo Simba, unaleta matumaini ya kufanya vyema na kufanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu.

 

“Ni jambo zuri ujio wa kocha mpya kwani amekuja kuongeza nguvu na rekodi zake zinaongea, inaonekana ni kocha bora na atatufanya tufike pale tunapopahitaji, hivyo wakiungana na huyu tuliye naye sasa Masoud Djuma tutafika mbali.“Tunamuomba Mungu aweze kutusaidia kufanya vyema katika mechi zetu zote ikiwa ni pamoja na kushinda mabao mengi ambayo yatatusaidia kuwa vizuri zaidi,” alisema Mkude.

 Khadija Mngwai, Dar es Salaam

Comments are closed.