The House of Favourite Newspapers

Maajabu ya Frirauni! Ukizikwa Unarudi Juu Kesho

0

UKISTAAJABU ya Musa utaona ya Firauni. Baadhi yetu tunamjua Musa ambaye Mungu akin‑ alia uhai huko mbele siku moja nitamzungumzia hapa, lakini uliwahi kujiuliza huyo Firauni ni nani hasa?

 

Fahamu tu kwamba Firauni ni babu yetu wa asili. Alikuwa ni mtu mweusi tii. Jina lake aliitwa Mkuu Ramesses wa II au Sese. Nimekuwa nikiona habari kuwa eti mwili wa Firauni huwa ukizikwa, unarudi juu ya ardhi kesho yake! Hivi inawezekanaje? Tena husemwa na watu wenye akili timamu kabisa, mimi siamini. Kiukweli haya ni maajabu makubwa mno

 

Hapa utaamini kuwa binadamu ni dhaifu mno kwenye imani. Ni rahisi sana kumteka mtu yeyote akili kwa kutumia kivuli cha imani. Gazeti la ­ UMAA limechimba kuhusu huyu Firauni, lakini kabla ya kusema ni nani hasa, tusikie habari zake za kuzikwa, kupotea kwa maiti yake kisha kupatikana tena baadaye.

 

Mwanzo huyu Firauni alizikwa katika Bonde la Wafalme huko Misri, lakini kwa sababu ya uporaji wa vitu vya thamani alivyokuwa amevishwa, makuhani walihamisha mwili wake kutoka eneo hilo na kuupeleka ndani ya kaburi la Malkia Inhapy.

 

Miaka mingi baadaye waliuhamishia tena mwili wa Firauni kwenye kaburi la Kuhani Mkuu Pinudjem II. Yote hii ni kwa sababu ya kuweka kumbukumbu. Kutokana na matetemeko ya ardhi ya miaka kati ya 1000 AD hadi 1500 AD, vitu vingi vilipotea huku baadhi ya makaburi mengi yakiharibiwa.

 

Baadhi ya makaburi, majumba na makumbusho mengine yalipotea ikiwa ni pamoja na mwili wa Firauni. Lakini mwanzoni mwa miaka ya 1800, mwili huo wa Firauni ulipatikana tena pembezoni mwa Bahari ya Shamu.

 

Cha ajabu ulikuwa haujaharibika kwa maana ya kuoza kwani ulionekana kama uliokuwa umekaushwa. Kuna madai kwamba, Firauni hakufa kwenye gharika ya Musa, mwili wake hadi sasa unathibitisha kuwa alikufa akiwa mzee wa zaidi ya miaka 80 kwa maradhi ya kawaida. Pia si mwili wa Firauni tu uliopo kwenye makumbusho ya Misri. Ni miili mingi ya Ma‑ rauni (mafarao) tofauti na baadhi ya watu walioishi kwenye Misri ya Kale.

 

FIRAUNI NI NANI?

Ma‑ rauni au Mafarao walikuwa wengi, lakini Firauni au Farao maarufu zaidi ni yule aliyekuwa mfalme wa pili wa uzao wa 19 wa familia ya kifalme nchini Misri. Alikuwa miongoni mwa Ma‑ rauni wenye nguvu kuwahi kutokea Misri.

 

Firauni huyu alipewa kiti cha ufalme mapema akiwa na umri wa miaka 20 tu na akaongoza miaka ya 1279 BC hadi alipofariki dunia baadaye miaka ya 1213 BC kwa maradhi ya mishipa na ini.

 

Firauni huyu aliongoza Misri kwa miaka 67 akiwa ni wa pili kuongoza kwa kipindi kirefu zaidi katika historia ya Mafarao. Mbali na vita, Firauni huyu anakumbukwa mno katika juhudi zake za utunzaji wa historia ya Misri katika mahekalu.

 

Kwa kumbukumbu nyingi muhimu zilizomo kwenye mahekalu, zana za kale, michoro na maandishi zinamfanya Firauni huyu kuwa mmoja wa Mafarao muhimu wa Misri ya Kale. Jeshi la Firauni huyu lilisaidia kulinda mipaka ya Misri kutoka kwa wavamizi na majambazi katika Meditrenian na Libya.

 

Pia Firauni huyu alifanya kampeni za kurudisha ardhi iliyokuwa imeporwa na wavamizi kwa kusaini mikataba ya amani kabla ya kutumia nguvu kuwapiga. Katika historia, Firauni alishindwa vita moja tu!

 

Vita inayokumbukwa ni ile iliyofanyikia Kadesh (Syria kwa leo) ya mwaka 1274 BC dhidi ya Wahiti. Ilikuwa ni vita kubwa iliyotumia zana za kisasa zaidi wakati huo katika historia ya vita za kale. Firauni alifanya makosa kwa kugawa vibaya vikosi vyake, jambo lililosababisha moja ya vikosi vyake kufyekwa wote! Hatimaye mpinzani akajitangazia ushindi na Firauni ikampasa kurudi nyuma kwa sababu ya kujiandaa kubaya na matatizo ya vifaa.

 

Vitabu kadhaa vya dini kama Biblia na Kurani vimekuwa vikizungumzia kifo chake katika hali ya kushangaza. Wao hudai kuwa Firauni ali‑ a kwenye maji wakati akiwafukuza Waisrael, lakini Wamisri wa kale wanapinga kabisa madai hayo na kudai Firauni alifariki dunia akiwa na umri wa miaka zaidi ya 87 kutokana na maradhi ya kibinadamu. Moja ya ushahidi ni wa mwili wa Firauni huyu ambao unaonekana wazi kuwa mtu huyo alifariki dunia akiwa mzee kabisa.

 

Pia jambo lingine la kujiuliza ni kuwa akina Musa wakati wakimkimbia Firauni na kuwa wameshafanikiwa kuvuka bahari, huku nyuma waliwezaje kumuona Firauni katikati ya kikosi cha askari wa Misri akifa maji? Hayo ni mambo yanayowatatiza wengi, huku wengine wakienda mbali zaidi kuwa mwili wa Firauni huwa hautaki kuzikwa.

 

Achana na mawazo machafu kwamba, Firauni ndiye aliyekuwa kinara wa dhambi ya ‘u‑ rauni’ na katili kuliko wote, lakini huyu ndiye mmoja wa mafarao muhimu zaidi nchini Misri na leo anakumbukwa kwa namna alivyojitolea kuitetea nchi hiyo.

Makala: Sifael Paul na Mtandao

Leave A Reply