The House of Favourite Newspapers

Maamuzi ya TCRA Kwa Mobeto, Irene Uwoya

Irene Uwoya

Msanii Irene Uwoya na mwanamitindo, Hamissa Mobetto,  wamewajibishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kosa la kuweka picha za nusu uchi mitandaoni kinyume na kanuni za maudhui mtandaoni za mwaka 2018.

 

 

 

Katika maamuzi yake na kwa kuzingatia utetezi wa Mobetto ambaye amesema picha hizo alizipiga mwaka jana nchini Kenya, TCRA imempa onyo la mwisho na kwamba akirudia, atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha, TCRA imemtaka kuweka tangazo kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwaomba msamaha Watanzania na kuwataka kutosambaza picha zake za nusu uchi.

Kwa Irene Uwoya, yeye pia amepewa onyo la mwisho kwa kuzingatia utetezi wake alioutoa, pia ametakiwa kuomba msamaha kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Comments are closed.