The House of Favourite Newspapers

Maandalizi ya Sensa 2022 Yaanza

0


Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dk Albina Chuwa amesema maandalizi ya sensa ya sita nchini yanaendelea kama ilivyopangwa. Dk Chuwa ameyasema hayo leo Julai 12, 2021 jijini Dodoma wakati wa kikao cha wadau kwa ajili ya kujadili dodoso la sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

 

Ameeleza kwamba dodoso hilo lenye maswali 94 lipo kwa ajili ya kuandaa mikakati na maswali yatayotoa mwelekeo kwa wananchi. Amesema kikao hicho ni mfululizo wa vikao na shughuli za maandalizi katika kuelekea kwenye zoezi hilo.

 

Amefafanua kwamba kikao hicho cha kwanza ni halali kwa mujibu wa sheria ya takwimu sura ya 30, kwamba kazi zote za takwimu ni lazima zihusishe wadau. “Hiki kikao ni maandalizi ya sensa ya Agosti mwaka ujao 2022. Aidha Agosti hii ya 2021 tutafanya sensa ya majaribio,” amesema.

Leave A Reply