The House of Favourite Newspapers

Mabao 54 yamtesa Mavugo Simba SC

0

MSHAMBULIAJI wa Simba, Lau­dit Mavugo, ana kazi kubwa ya kuifikia rekodi yake ya kufunga mabao 62 ndani ya misimu miwili aliyotoka nayo katika Klabu ya Vital’O ya Burundi kabla ya kutua Simba.

Mavugo ambaye alijiunga na Simba msimu uliopita, aliondoka Vital’O akiwa na rekodi ya kufunga mabao 62 ndani ya misimu miwili na kuibuka mfungaji bora wa ligi ya kwao Burundi. Msimu wa kwanza alifunga mabao 32, wa pili 30.

Mshambuliaji huyo ambaye alitajwa kuwa moto wa kuotea mbali ambapo akiwa na Simba, msimu wa kwanza kwenye ligi alifunga mabao saba pekee hali iliyosababisha kuombewa muda zaidi kwa ajili ya kuzoea ligi ya Tanzania ambayo ni tofauti na sehemu aliyokuwa akicheza awali.

Katika msimu huu ambao ni wa pili kwa Mavugo mpaka sasa amefunga bao moja katika mchezo dhidi ya Stand United ikiwa ni mechi ya tano kwa mzunguko wa kwanza huku akishindwa kufunga katika nne za kwanza ambazo ni Simba 7-0 Ruvu, Azam 0-0 Simba, Simba 3-0 Mwadui na Mbao 2-2 Simba.

Kutokana na rekodi yake ya nchini Burundi ambayo alifunga mabao 62, mshambuliaji huyo ana deni la kuhakikisha anafunga mabao 54 ili kuifikia rekodi yake kitu ambacho huenda kikashindwa kutokea kufuatia uwepo wa washambuliaji wengine wakali ambao ni John Bocco na Mganda, Emmanuel Okwi.

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Leave A Reply