MAREKANI: Staa wa kikapu nchini Marekani katika Ligi ya NBA, LeBron James ameiongoza timu yake ya Cleveland Cavaliers kutembelea ikulu ya nchi hiyo kutokana na kutwaa ubingwa NBA msimu uliopita.
Obama akikabidhiwa jezi ya Cleveland.
Wachezaji wakipiga selfie mbele ya jengo la Ikulu. LeBron James akipiga selfie na mke wa Obama.
Michelle Obama akitaniana na wachezaji wa Cleveland.
James alikuwa ni sapota wa Hillary Clinton katikauchaguzi wa rais, lakini Donald Trump ndiye aliyeibuka mshindi.
Wakiwa ikulu jana Alhamisi wachezaji wa timu hiyo walijumuika na rais wa nchi hiyo, Barrack Obama na mkewe, Michelle Obama ikiwa pia ni sehemu ya kumuaga kabla hajaondoka madarakani kumpisha Donald Trump ambaye amechaguliwa katika uchaguzi wa rais ulifanyika wiki hii.
Imekuwa ni kawaida timu inaposhinda NBA kupata nafasi ya kwenda kutembelea mjengoni hapo maarufu kwa jina White House.
Katika hotuba yake aliyoitoa kwa wachezaji hao, Obama alimsifia James kwa kuonyesha uwezo wa juu na kueleza kuwa ni mchezaji ambaye hana ubinafsi anapenda mafanikio ya wengi, anajituma na ana nidhamu ya kazi.
Comments are closed.