Mtoto wa bondia na bingwa wa zamani wa UFC Francis Nganou afariki akiwa na miezi 15
Mtoto wa umri wa miezi 15 wa bondia Francis Ngannou amefariki dunia.
Bingwa huyo wa zamani wa UFC alichapisha kwenye X siku ya Jumatatu usiku: “Ameondoka mapdema, lakini bado ameenda.
“Mtoto wangu, mwenzangu, mwenzangu Kobe alijawa na maisha na furaha, sasa analala bila uhai. Nilipiga kelele jina lake mara kwa mara lakini hajibu.
“Nilikuwa mtu mwenye furaha karibu naye na sasa sijui mimi ni nani. Maisha sio sawa kutuathiri pale ambapo inaumiza zaidi.”
Meneja wa mpiganaji huyo Marquel Martin alichapisha mtandaoni akisema kwamba yeye pamoja na “mamilioni ya wengine” watamwombea raia huyo wa Cameroon.
Conor McGregor alikuwa miongoni mwa wapiganaji na mashabiki waliotuma salamu zao za rambirambi kwa bondia huyo mwenye umri wa miaka 37 na nyota wa zamani wa (MMA).
“Samahani sana kusikia kufiwa kwako Francis, sala zangu ziko pamoja nawe na familia yako kwa wakati huu,” Alisema raia huyo wa Ireland katika X.
Pambano la mwisho la Ngannou lilikuwa kushindwa kwake na Anthony Joshua huko Saudi Arabia. Baada ya pambano hilo alitupilia mbali pendekezo la kurudi kabisa katika MMA ambapo alitengeneza umaarufu wake.