The House of Favourite Newspapers

Machozi Ya Offset Kwa Cardi B, “Nimekuaibisha, Naomba Nisamehe” (VIDEO)

 

Baada ya Cardi B kuachana na rapa Offset toka kundi la Migos Disemba 5 mwaka huu, Offset amerudi kwenye vichwa vya habari akimuomba msamaha mke wake huyo kwa aliyoyatenda na kumwahidi kutorudia tena.

 

Kupitia video katika akaunti ya Offset ya instagram inamwonysha akisema, “Ninataka kumtakia siku ya kuzaliwa mke wangu Cardi.Tumepitia mambo mengi mpaka wakati huu, nimekutia aibu, nimekufanya upate ghazabu.Nilikuwa katika shughuli zangu lakini sikutaka kujipata katika shughuli hii na naomba unisamehe.Kwa kuvunja moyo wako, kwa kuvunja ahadi yako, kwa kuvunja ahadi ya Mungu, kwa kuwa mbinafsi na mwanaume mwenye makosa.Najitahidi kuwa mtu mwema.nataka kutua mzigo huu toka kwenye mabega yangu.Nakuomba msamaha Cardi, ‘nakupenda’.

 

Offset aliendelea kuomba msamaha huku akitaka afurahie sikukuu ya Krismas pamoja na mwanaye wa miezi minne ‘Kulture’ , “ Kulture nataka kufurahia sikukuu ya Krismas na wewe.Nataka niwe naweze kuishi na wewe maisha yangu yote, naomba nisamehe kwa yote yaliyotokea, sikuwa na hisia zozote na Yule mwanadada nilikuwa namfurahisha tu.Nimekuomba msamaha na nakupenda na natumaini umenisamehe.”

 

Hakuna muitikio wowote wa Cardi B mpaka wakati huu kuhusiana na na kauli ya msamaha ya mume wake Offset.

 

ITAZAME VIDEO HAPO CHINI

F O R G I V E M E @iamcardib A L L I W A N T F O R M Y B D A Y

843.1k Likes, 86.9k Comments – OFFSET (@offsetyrn) on Instagram: “F O R G I V E M E @iamcardib A L L I W A N T F O R M Y B D A Y”

Comments are closed.