The House of Favourite Newspapers

Madai ya Kuringa, Rammy Awa Mbogo

Rammy Galis

MUGIZAJI wa kiume Bongo, Rammy Galis amefunguka kuwa anachukizwa na minon’gono ya watu wanaombeza kuwa anaringa kitu ambacho kinamkera sana kwa sababu hayuko hivyo.

Akizungumza na Amani juzikati, Rammy alisema kuwa kawaida yake yeye ni mkimya sana na hupenda kuzungumza pale anapokutana na mtu ambaye wamezoeana ambapo ana uhuru wa kuzungumza naye chochote lakini kinyume na hivyo anamheshimu kila mmoja.

“Mara nyingi nilishasikia watu wakisema mimi naringa au nina dharau kitendo ambacho kinanikera sana kwa sababu mimi siko hivyo kabisa labda ukimya wangu wanaona ndiyo niko hivyo lakini sivyo alisema Rammy.

Comments are closed.