The House of Favourite Newspapers

Madee: Afunguka Sababu Kukaa Kimya ‘Sijaacha Muziki’

0
HAMAD Ally au Madee, Rais wa Manzese Music; ni muda sasa umepita tangu aachie ngoma yake ya Hadithi ambapo hatimaye anafunguka sababu iliyomfanya akae kimya kwa muda wote huo bila kuachia ngoma nyingine huku akiwa hana papara kabisa.
Akizungumza na IJUMAA SHOWBIZ, Madee anasema kuwa, alikaa kimya kwa kipindi kirefu kwa sababu ya matatizo ya kifamilia ambayo alikuwa nayo, lakini pia hiyo haimfanyi yeye kuwa na haraka ya kutoa ngoma kila siku kwa sababu anaamini ngoma zake huwa zinaishi hivyo hata akitoa mara mojamoja siyo mbaya.
 
 
“Nilipata matatizo kidogo ya kifamilia ambayo ndiyo yalinifanya nikae muda mrefu bila kuachia ngoma, lakini pia sasa hivi tena tunakaribia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hivyo inabidi tena tusubiri uishe, mbali na yote hayo bado sina papara ya kuachia wimbo mpya kwa sababu naamini nyimbo zangu huwa zinaishi kwa hiyo hata nikae muda gani bado zitaendelea kufanya vizuri na napata shoo za kutosha,” anasema Madee.
Leave A Reply