The House of Favourite Newspapers

Madereva Waliotekwa Na Waasi Nchini DRC, Waachiwa

whatsapp-image-2016-09-15-at-8-34-33-am-750x375Baadhi ya malori yaliyochomwa moto na waasi hao siku walipowateka madereva.

Chama cha Wasafirishaji wa Malori nchini Tanzania – TATOA kimesema madereva wote waliotekwa na waasi wa Mai Mai huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameachiwa huru kufuatia juhudi zilizofanywa na jeshi la Kongo.

Chama hicho pia kimesema kuwa hakuna pesa yoyote iliyolipwa kama kikombozi kwa waasi hao.

Makamu Mwenyekiti wa TATOA Bwana Eliasi Lukumay amesema mara baada ya kuachiwa kwa madereva hao, jeshi la Kongo limeufunga kwa muda mpaka baina yake na Rwanda, eneo ambako utekaji huo umefanyika na kwamba hakuna lori lolote la mizigo linaloruhusiwa kupita katika eneo hilo.

Bw. Lukumay ameitaja kampuni ya Kitanzania iliyoathiriwa na utekaji huo kuwa ni ya Simba Trucks inayomilikiwa na mfanyabiashara Azim Dewji na kwamba hatua ya kufungwa kwa muda kwa eneo ulipotokea utekaji huo haiepukiki kwa sasa na kwamba kama wasafirishaji wanashughulikia kwa karibu hatma ya madereva waliopo nchini Kongo kwa sasa na wale waliopo njiani wakisubiri kuvuka eneo hilo.

 

 

Comments are closed.