Madhara ya kunywa pombe
Pombe ni kati ya vinywaji watu wengi wamekuwa wakipenda kutumia kama moja ya starehe au katika sherehe.
Pombe Alcohol ni aina ya kampaundi iitwayo ethanol ambayo huweza kuathiri ufanyaji kazi wa ubongo Psychoactive.
Pombe hupatikana katika vinywaji mbalimbali kama bia (zikiwa na asilimia 3-8 ya pombe), mvinyo ambayo hutengenezwa kutoka na zabibu ukiwa na asilimia 9 – 14 ya pombe, pombe kali kama gin, whiskey, brandy na tequilla zina asilimia 35 – 50 ya pombe pia kuna gongo na pombe za kienyeji.
Mtu anapokunywa pombe, asilimia 20 ya pombe iliyonywewa hunyonywa tumboni na 75 nyingine hunyonywa na utumbo mdogo kisha huingia katika damu. Pombe hunyonywa kwa haraka kama tumbo halina chakula.
Kwenye damu husambaa mwilini na kiasi kikubwa cha pombe huvunjwavujwa kwenye kampaundi nyingine Metabolised na ini kisha kutolewa na figo kama mkojo, pia kwenye hewa mtu anayotoa nje na kiasi kidogo katika jasho.
Ini huweza kuvunjavunja kiasi kidogo cha pombe kwa wakati, hivyo kiasi kinachobaki kama mtu amekunywa pombe nyingi huendelea kuzunguka mwili mpaka kitakapovunjwavunjwa.
Pombe huathiri kila kiungo kwenye mwili, kuanzia ubongo hadi misuli ya mwili. Ikiingia kwenye ubongo, pombe huenda kuzuia kemikali Neurotransmitters zinazofanya ubongo uwe active kama glutamate na kuruhusu kemikali kama GABA ambazo huufanya ubongo ufanye kazi taratibu. Pia huongeza dopamine ambayo huleta hali ya furaha.
MADHARA YAKE
Madhara ya unywaji wa pombe kwenye afya ya mwanadamu hutegema na mtu, mazingira ya unywaji na kiasi cha pombe anachokunywa.
Kiasi cha pombe alichokunywa mtu ndiyo kinadhuru mwili, siyo aina ya pombe kwani hupunguza uwezo wa kufikiri na uharaka wa kuchukua maamuzi wakati wa dharura.
Watu ambao hawaruhusiwi kunywa pombe kiafya ni mtu yeyote aliye chini ya umri wa miaka 18, mjamzito, mtu anayekunywa dawa zinazoingiliana na pombe.

