The House of Favourite Newspapers

Madhara Yatokanayo Na Vyombo Vya Plastiki!

 

USITUMIE  kabisa vyombo vya plastiki kuchemshia au kuwekea vyakula vya moto kama chai, maziwa, supu, maji, ugali n.k.

 

Ugunduzi mpya ambao umethibitishwa hivi karibuni ni kwamba, plastiki inapopata moto huzalisha kemikali iitwayo BPA (Bisphenol A) ambayo ikiingia mwilini husababisha magonjwa mengi kwa binadamu, miongoni mwake ni:

  1. Magonjwa ya ini
  2. Magonjwa hatari ya moyo
  3. Kisukari
  4. Magonjwa ya kizazi kwa jinsia zote
  5. Kuathirikw kwa nguvu za kiume
  6. Pumu huongezeka kwa wagonjwa wa pumu
  7. Huathiri mfumo wa fahamu na kusababisha kupoteza kumbukumbu.

 

Tujikumbushe:

 

Zamani mababu zetu walikula vitu vya asili na kutumia vitu vya asili,  ndiyo maana hawakuwa wanaumwa magonjwa ya ajabu-ajabu.

 

Mababu zetu  waliishi miaka mingi kwani hawakuwa na vyakula vya viwandani, yaani vyakula vyenye kubuniwa na kutengenezwa na binadamu, ambavyo ni vyakule vyenye kemikali za sumu.

 

Vyakula hivyo vinaweza kuliwa lakini ni muhimu kuzingatia  unywaji wa maji mengi ambapo kiwango cha chini ni lita moja kwa siku.  Pia ni muhimu kula  matunda mengi na mboga za majani.

 

TAHADHARI

 

Hakikisha huweki vyakula vya moto kwenye vyombo vya plastiki nyumbani kwako na badala yake tumia vyombo vya udongo ambavyo bei yake ni ya chini.

Pia jitahidi uwafikishie taarifa hii walezi wa familia — mama na baba — sehemu mbalimbali, kwani wengi hawana elimu hii.

  

KUMBUKA

 

Madhara ya plastiki huonekana baada ya muda mrefu ambapo unaweza kuvitumia vyombo hivyo na kutoona madhara yake katika muda mfupi lakini baada ya miaka ipatayo kumi utapata ugonjwa ambao utashindwa kujua chanzo chake. Wengine watasingizia uchawi kumbe mchawi ni mikono yako!

 

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.