The House of Favourite Newspapers

Madiwani Kulipwa Posho Kila Mwezi- Rais Samia

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan,  amesema kuwa serikali imeridhia madiwani kulipwa posho ya kila mwezi ili iwasaidie kuacha kuhangaika kukusanya fedha kwenye Halmashauri.

 

Ameyasema hayo leo Septemba 27 , akiwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania-ALAT, unaofanyika kwenye ukumbi  wa Jakaya Kikwete Convention Center, Jijini Dodoma.

 

“Kwenye bajeti ya mwaka huu, Serikali imeridhia madiwani kuanza kulipwa posho ya kila mwezi, na hii itasaidia madiwani kuacha kuhangaika na pesa inayokusanywa kule ili wajilipe posho, posho yenu sasa imehakikishwa ipo.”

 

“Kwa kadri uwezo wa Serikali utakavyokuwa ukiongezeka tutaangalia kuboresha maslahi ya madiwani na watendaji wengine kwenye halmashauri zetu.” ameongeza Rais Samia.

Leave A Reply