The House of Favourite Newspapers

Madiwani wa Viti Maalum Dar, Wacharuka Kupinga Ukatili wa Kijinsia Nchini(PICHA+VIDEO)

0

 

MADIWANI wa vita maalum katika Mkoa wa Dar es Salaam wamesimama kidete kupinga ukatili unaoendelea dhidi ya watoto wakiomba Mamlaka zinazohusika kuhakikisha wanatunga sheria kali ambazo zitawaadhibu wale wote watakaokutwa na hatia dhidi ya manyanyaso kwa watoto ikiwemo vitendo vya ulawiti.

Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Kinondoni Rehema Mandingo

Akiongea kwa niaba ya madiwani wa Viti Maalum ambaye ni Diwani wa Viti Maalum katika Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam amesema madiwani wote kwa ujumla wanaunga juhudi zinazofaywa na Dkt Dorothy Gwajima ambaye ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Watoto katika kutetea haki za watoto ikiwemo kukemea unyanyasaji wa kijinsia pamoja na ukatili wa watoto.

 

Mandingo ametoa rai kwa madiwani wote nchi nzima kuungana na kupaza sauti kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia katika jamii zetu.

Madiwani wa Viti Maalum wamejitokeza kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto

Matukio yanayoendelea nchini kwa sasa Diwani Mandingo ameyaita kama Janga la Kitaifa huku akiwaomba viongozi wa dini kumuombea Rais Samia pamoja na jamii kwa ujumla ili kupambana ma matukio ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.

Diwani wa Viti Maalum Kata ya Kiwalani jijini Dar es Salaam Moza Mwano

Lakini pia ametoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla kwa kazi yake anayoifanya ndani ya Mkoa huo lakini pia ametoa shukrani za pekee kwa Jeshi la Polisi ambalo linafanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha jamii inaishi katika misingi ya ubinadamu.

 

Naye Diwani wa Viti Maalum Kata ya Kiwalani jijini Dar es Salaam Moza Mwano ametoa rai kwa wazazi kuwa makini kwenye vipindi vya kwenye Luninga wanavyoangalia watoto wao kwani kuna vipindi vingine havina maadili ambavyo vinaletwa na Mataifa ya Magharibi ambavyo kimsingi vinaharibu mila na desturi za kitanzania.

Leave A Reply