The House of Favourite Newspapers

Maelfu Waandamana Kupinga Sheria za Corona

0

WATU 3,000  wameandamana nchini Italia kupinga sera za afya za serikali wakati kukianzishwa sheria kali za kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

 

Shirika la habari la ANSA limeripoti kuwa watu walikusanyika kwa maandamano dhidi ya cheti cha kidigitali cha Corona cha Umoja wa Ulaya kinachojulikana nchini humo kama pasi ya kijani Green Pass).

 

Kuanzia Agosti 6, watu watahitajika kutoa uthibitisho wa chanjo, matokeo yanayothibitisha kutoambukizwa virusi hivyo ama ushahidi wa kupona baada ya maambukizo ili kuweza kushiriki katika dhifa za chakula za ndani ama kuingia katika maduka na mabwawa ya kuogelea miongoni mwa maeneo mengine ya umma.

 

Gazeti la Corriere della Sera limeripoti kuwa maandamano yalifanyika katika miji ya Milan,Turin na Naples.

 

Hivi karibuni, serikali ya Italia imeimarisha hatua za kupambana na ongezeko la visa vya maambukizo ya virusi vya corona huku ikiweka masharti makali kwa mikusanyiko kwenye maeneo ya ndani.

 

Leave A Reply