The House of Favourite Newspapers

MAGAZETI YA GLOBAL YAPIGA HODI CHANIKA

Afisa Usambazaji wa Global, Charles Mponzi (katikati) akigawa vipeperushi vya magazeti ya Global.

Kikosi cha mauzo cha Kampuni ya magazeti ya Global Publishers, leo kiliingia tena mitaani kuyanadi magazeti ya Risasi na Championi ambapo sasa kikosi hicho kilipiga hodi mitaa ya Gongo la Mboto, Pugu, Kigogo Fresh mpaka Chanika na kuyanadi magazeti hayo.

Msomaji huyu alinaswa akiwa makini na gazeti la Championi maeneo ya Chanika Mwisho.

Wakazi wa maeneo hayo walionekana kuvutiwa na magazeti ya Risasi na Championi na wengi wao wakayachangamkia kwa kuyanunua magazeti hayo ambayo yana habari za uhakika na zenye manufaa makubwa kwa jamii.

Mussa Mgema wa Global (kushoto) akimuelekeza jambo msomaji.

Akizungumza na wakazi wa maeneo hayo, Ofisa Usambazaji wa Global Publishers, Charles Mponzi, amewataka wananchi hao kuendelea kununua magazeti ya Global ambayo ni Uwazi, Championi, Risasi Jumatano, Ijumaa Wikienda, Amani, Ijumaa, Risasi Jumamosi ambayo huuzwa kwa shilingi 800.

Msomaji wa Kigogo Freshi akiwa makini kusoma gazeti la Risasi Jumatano.

Aidha, Mponzi amewataka pia kununua Gazeti la Spoti Xtra ambalo hutoka kila Alhamisi na Jumapili kwa Tsh 500 tu na kushiriki promosheni katika kuponi iliyopo ukurasa wa pili ambapo msomaji atajishindia jezi orijino ya timu kubwa za Ulaya.

Wasomaji wa Gongo la Mboto wakifurahia uhondo wa magazeti ya Global, Risasi na Championi.

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL   

Comments are closed.