The House of Favourite Newspapers

Ibada ya Kuaga Mwili wa Isaac Gamba, Bunda – Pichaz

Wanakwaya Kanisa la Waadventista Wasabato wakiimba wakati wa ibada ya kuaga mwili wa Isaac Gamba, Bunda, Mara leo Jumatano kabla ya mazishi.

MWILI wa aliyekuwa mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) nchini Ujerumani, Isaac Muyenjwa Gamba umeagwa katika ibada ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo Jumatano, Oktoba 31, 2018 nyumbani kwao, Bunda mkoani Mara.

Waombolezaji wakiwa msibani.

Mwili wa Gamba ambao uliwasili nyumbani kwao jana nyumbani kwao Bunda kwa ajili ya amzishi ukitokea Dar es Salaam kupitia Mwanza.

Jeneza lenye mwili wa marehemu Isaac Gamba likitolewa nje kwa ajili ya ibada ya kuagwa nyumbani kwao leo.

Mazishi ya Gamba yanatarajiwa kufanyika leo kwenye makaburi ya familia yao yaliyopo nje kidogo ya Mji wa Bunda.

Jeneza lenye mwili wa marehemu Isaac Gamba likitolewa nje kwa ajili ya ibada ya kuagwa nyumbani kwao leo.

Viongozi mbalimbali wa vyama na siasa wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, Katibu Mkuu wa Chadema -Zanzibar, Salum Mwalimu na wengine wamejitokeza na kuungana na wanafamilia pamoja na waombolezaji wengine kuaga mwili wa marehemu.

Jeneza lenye mwili wa marehemu Isaac Gamba likitolewa nje kwa ajili ya ibada ya kuagwa nyumbani kwao leo.

Gamba alikutwa akiwa amefariki chumbani kwake Alhamisi, Oktoba 18, mwaka huu, jijini Bonn nchini Ujerumani alikokuwa akifanya kazi zake.

Mama mzazi wa Isaac Gamba, Bi. Rachel Muyenjwa Gamba akiketi.

Baada ya uchunguzi wa hospitali nchini Ujerumani, imegundulika kuwa kilichosababisha kifo chake ni kuvuja kwa damu kwenye ubongo (Brain Hemorrhage) yaani presha ya damu.

Mama mzazi wa Isaac Gamba akiwa mwenye huzuni wakati wa ibada ya kuaga mwili wa mwanaye kanisani leo.
Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili amesma kuwa kifo cha Isaac Gamba kiwe funzo kwa Watanzania waishio ughaibuni kuwa wanapaswa kuiga mfano wake wa yale aliyoyafanya akiwa nchini ujerumani ya kuhabarisha umma kuendana na taaruma yake.

Akitoa salam za pole Bupilipili ameushukuru uongozi wote wa DW kwa kufanikisha shughuli zote za kuuleta mwili wa marehemu hadi kufika mjini Bunda na watu wote waliohakikisha mwili huo unafika salaama na kuwafariji familia.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili akitoa salamu za pole kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.

 

Salum Mwalimu akitoa naye salamu za pole kwa niaba ya chama cha demokrasia na maendeleo chadema Mjini Bunda.

PICHA NA DENIS MTIMA

MASKINI! Sam Mahela ashindwa kujizuia, Amwaga Machozi!!

Comments are closed.