The House of Favourite Newspapers

Magereza Yaliyogeuzwa Kuwa ‘Machinjio’

0

Katika historia ya uhalifu kuna maeneo ambayo huwa hayazingatiwi sana kama hatima ya watu wanaokamatwa kwa makosa mbali mbali . Maeneo hayo ni magereza ambayo hata wasiokuwa na hatia hujikuta wamewekwa ndani na wengine hata kufa wakiwa jela.

 

Kila nchi ina magereza yake ya vitengo mbali mbali kulingana na wahalifu wanaozuiliwa .hata hivyo kuna baadhi ya magereza yaliyojipa sifa mbaya na ya kuogofya katika miaka ya hivi karibuni kwa sababu ya mateso , hali mbaya ya maisha na hata maafa.

 

Baadhi ya mageeza hayo yalikuwa ni kazi ya viongozi madiktea waliohitaji ngome za kuwaangamiza wapinzani wao na kuwazuilia wafungwa wa kisiasa.

 

Mengine yalikuwa ni kwa sababu ya vita na kando na magereza yanayotambulik ama kama hatari zaidi duniani kama vile gereza la Tadmor , La Sabaneta, La Sante, Alcatraz , Rikers na Guantanamo bay ,haya hapa magereza matatu ambayo kama jamaa yako angeshikwa kupelekwa ndani ungekata tamaa ya kuwahi kumuona akiwa hai tena.

Waliobahatika kutoka wanajua kwamba wana bahati sana .

Abu ghuraib – Iraq

Gereza hili lilikuwa viungani mwa mji wa Baghad nchini Iraq. Gereza la Abu Ghraib lilijipata katika umaarufu ulimwenguni kwa sababu mbaya baada ya kubainika kuwa vikosi vya usalama vya Marekani viliwatesa wafungwa kwa kinyama

 

Mnamo 2004, mwaka mmoja baada ya uvamizi wa Marekani huko Iraq, picha za kushangaza za wafungwa wa Iraqi waliokuwa uchi huku wakihangaishwa kwa kuwekwa juu ya dari zilianza kusambazwa katika vyombo vya habari vya kimataifa.

 

Wafungwa wengine walionyeshwa wakiwa wamefungwa kwa nyaya za stima wakifanyiwa madhila kutumia umeme . Yote yalikuwa yakifanyika huku wanajeshi wa Marekani wakionekana kufurahia vitendo vyao hivyo.

 

Huu ulikuwa mwanzo wa kashfa ya gereza la Abu Ghraib ambalo mwishowe lilimlazimisha rais wa wakati huo wa Marewkani George Bush kujiokeza na kuomba msamaha

Mnamo Julai 21, 2013, muda mrefu baada ya operesheni ya Abu Ghraib kurudi kwa Wairaq, shambulio la kigaidi la kiwango ambacho hakijawahi kutokea lilifanyika katika gereza hilo , na kusababisha wafungwa zaidi ya 500 kutoroka. Baadhi ya waliotoroka wanaaminika kuwa walijiunga na tawi la al-Qaeda lililohusika na kuzuka kwa mashambulizi zaidi na kuchipuka kwa kundi la Islamic State.

 

Mnamo Aprili 2014 -Serikali ya Iraq gererza hilo la gereza hilo la Abu Ghraib kwa sababu ya kile ilichosema ni hofu ya usalama.

 

Wafungwa wake 2,400 walihamishwa hadi katika magereza mengine katika mikoa ya kati na kaskazini. Gereza hilo sasa linaitwa Baghdad Central Prison na wafungwa kadhaa wanaaminika kufariki humo wakati wa utawala wa Saddam Hussein

 

Abu salim -Libya

Mamo mwaka wa 2011 kupatikana kwa kile kilichoaminika kuwa kaburi la pamoja la zaidi ya wafungwa 1,200 waliouawa katika jela ya Tripoli ya Abu Salim mnamo 1996 kuliibua kumbukumbu zenye uchungu kwa wale ambao walisubiri miaka kufahamu hatima za wapendwa wao.

 

Kaburi hilo lilifungua majonzi ya wnegi kuhusu hali ilivyokuwa katika gereza hilo .

Baadhi ya vipande vya mifupa ya watu vilipatikana vimetapakaa katika maeneo kadhaa.

 

Eneo hilo ndilo maafisa wanadhani wafungwa wengine 1,270 walizikwa baada ya kile kinachojulikana kama mauaji ya Abu Salim, mojawapo ya visa vya kutisha kabisa vya utawala wa Kanali Gaddafi.

Chini ya utawala wa Gaddafi, Abu Salim mara nyingi ilikuwa ndio makao ya wafungwa wa kisiasa, wanaodaiwa kuwa itikadi kali za kidini na wapinzai wake.

Alisema tindikali /asidi ilimwagwa juu ya shimo kisha lingefunikwa kwa lami.

 

Familia za wahanga wa 1996 kwa muda mrefu walikuwa wakingoja majibu na siku hiyo walikumbana na kile walichohofia sana -kwamba jamaa zao waliokuwa wamekamatwa waliuawa. Walikuwa matajiri kuliko hata baadhi ya nchi, lakini pesa zao zilitoka kwa uhalifu

Jinsi Bin Laden, Saddam na Gaddafi walivyosakwa na kukamatwa au kuuawa

Mtu mmoja aliyekuwa msaidizi wa Gadhafi aliyezuiliwa baada ya kuporomoka kwa utawala wake alidai kwamba maiti zilitupwa ndani ya shimo lililochimbwa ndani ya eneo la gereza. Alisema tindikali /asidi ilimwagwa juu ya shimo kisha lingefunikwa kwa lami.

 

Ilichukua karibu miaka kumi kabla ya utawala wa Gadhafi kukiri hadharani kwamba mauaji yalifanyika katika gereza hilo. Wakati wote huo, familia za wafu ziliendelea kupeleka chakula kwa wapendwa wao ambao waliamini kuwa wako hai.

 

Carandiru -Brazil
Gereza la Carandiru nchini Brazil liligonga vichwa vya habari oktoba mwaka wa 19192 wakati wafungwa walipofanya maandamano wakitaka kutoroka baada ya kutokea ugomvi kati ya wawili kati yao .

 

Polisi wa gereza hilo walitumia nguvu kupindukia ili kuzima vurugu hizo na kusababisha wafungwa 111 kufariki . Gereza hilo lilikuwa mojawpao ya magereza makubwa sana Marekani kusini na lilikuwa na wafungwa 10,000 . Kilichofuatia baadaye mwaka wa 2013 ni kushtakiwa na kupewa hukumu ya miaka mingi polisi waliohusika na mauaji ya wafungwa hao .Gereza lenyewe lilifungwa mwaka wa 2002.

 

Maafisa 25 wa poilisi walihukumiwa kifungo cha miaka 624 kila mmoja kuhusiana na mauaji hayo lakini nchini humo hakuna anayeweza kuhudumu kifungo cha Zaidi ya miaka 30.

 

Chini ya sheria za Brazil hakunaanayefaa kupewa hukumu ya maisha jela na hakuna mtu alityetuhumiwa anayeweza kuhudumu kifungo cha Zaidi ya miaka 30 jela.

Leave A Reply